Hivi majuzi nimeota ndoto imenishangaza

Lotus 123

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2021
Posts
3,151
Reaction score
5,513
Nimeota nimekutana na malaika watu, hilo halikunishutua sana mimi ni mpentecostal safi. Cha ajabu hawa malaika walisema wanatoka kwa suba(Mungu wa Islam) na wametumwa kwa baba yangu?

Hii inaweza kuwa na maana gani? Kwa kifupi kabisa mimi sijawahi hata kuwaza kuwa kwenye Imani hiyo. Je, hawa malaika ni akina nani?
 
Ila uislam una undugu na majibu. Chukua tahadhari. Fanya maombi.
 
We mlokole gani usiyemjua Mungu wa waislam? Mungu wa waislam ni ALLAH. Huyo msuba ni Mungu wenu huko
 
Ila uislam una undugu na majibu. Chukua tahadhari. Fanya maombi.
Yeah, "majibu" yote kuhusu maisha ya mwanadamu na namna ya kumcha Mungu yapo katika Uislamu. Umeongea vizuri kabisa bila kutarajia........neema za Allah hizo kuwapiga 'dafrao' wenye chuki dhidi ya Uislamu. MashAllah
 
Fanya maombi kabla ya kulala, Mwombe Mungu airudie ndoto hiyo Leo na akupe maana yake.

Aombacho mtu hupewa.
 
Ndoto hazina maana yoyote ni upuuzi tu kama upuuzi mwengine

Siku nitayozingatia walau kiasi kuhusu ndoto ni siku ambayo;

Nitaota ndoto ambayo itajirudia vile vile zaidi ya mara moja katika vitu ambavyo sijawahi kukutana navyo kwenye maisha yangu ya kawaida

(sio naota zombi wakati naliona kwenye movie, au ndugu yangu ambae kila siku napishana nae kitaa)

Kidogo itamake sense. . .
 
Karibu sana, anza kujifunza uislam, usiangalie waislam, utaupenda
 
Unampotosha mwenzako aabudie sanamu kijana na kufanya shirki kwa Mungu ambayo ndio dhambi kubwa kuliko yeyote ile
 
Huyo si malaika ni jini. Sasa wewe endekeza likutie kwenye kuabudu majini.
 
Hata wewe hujachelewa maana dini ya kweli ni Uislamu
Ukiona dini unayoiamini haiamini Juu ya Yesu kuwa mkombozi wa ulimwengu na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu toka huko haraka na usigeuke nyuma!!

Ukiona unaeamini ndio mwokozi wako kalala mauti basi tambua hana cha kukusaidia njoo kwa Yesu alie hai Mbinguni
 
Kumbe Mungu wao anaitwa suba?
 
omba sana na ukemee Roho ya umauti inakuzengea...

kemea sana roho za kichawi na kishirikina zinakufuata kwa nguvu sana...

that is arlert...

R.I.P Laigwanan comrade ENL
 
Utakuwa Kwenye Mahusiano Na Mwanamke Wa Imani Tofauti Na Wewe Na Itakutaka Kati Yenu Mmoja Aache Imani Anayoiamini.
 
Suba Mungu wa waislam.??
Ww itakuwa umechanganya, msuba ni mungu wa marasta kina Bob πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Hebu vuta halafu ulale tena utaniambia
 
Sasa haoni kama tungekuwa tunaota vitu ambavyo hatuvijua kabisa ndio ndoto zingekuwa hazina maana?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…