Tutaacha lini ku assume?
Michango mingi hapa JF kuhusu mama Salma imelenga kumbeza kwamba hajui hiki wala kile.Kwa wale wasiomfahamu kwa karibu naomba mfahamu machache kumhusu huyu mama:
1. Ni mama mwenye elimu yake inayomtosha kuenea kwenye hicho kiti cha u first lady ( FL hupatikani by virtue of a woman's marriage kwa mkuu wa nchi na siyo kwa kuapply, kufanya interview, kuonyesha makaratasi - academic credentials, au kuonyesha uzoefu)
Mama Salma ni mwalimu wa shule ya msingi, na nasikia hana uwezo wa kufundisha zaidi ya darasa la nne. Kwa maana hiyo atakuwa mwalimu wa cheti, yawezekana daraja B. Kigezo cha kuwa 1st lady ni kuwa mke wa rais wa nchi basi.
2. Mama wa kwanza anajua kiingereza as a third language kama walivyo watanzania wengi including walio members JF.So kusema ati hajui kilichoandikwa kwenye mtandio wake si sahihi.Wengine hubeza wenzao bila sababu..afterall kiingereza ni lugha tu kama lugha nyingine hakuna cha ajabu kukijua.Kuna mtu anajua kiingereza lakini substance kwenye analoongea ni almost 0!
Thread haingolei kuwa anajua au hajui Kiingereza, bali je, ujumbe alioubeba na kuwafikishia wageni kutoka US ni kweli. Sio kwamba amebeba ujumbe hasioufahamu. Ungeweza kuwaambia wachangiaji wasitoke nje ya mada. Kwa kifupi Kiingereza hakifahamu vizuri na ndio maana JK alipokaribia au alipopata urais mama JK alipewa crash course ya Kiingereza! Kwanza wewe ndio umeleta mada tofauti na mpya kabisa! Ungekuwa unajibu mtihamu matokeo yako ni ZERO.
3. Huyu mama anafanya mengi makubwa hasa kwenye elimu ya wasichana na kupambana na UKIMWI.Tumpe heshima yake.
Elimu ya wasichana ndio elimu gani hiyo? Elimu ya uzazi? Au msichana alivyo? Au unamaanisha 'wanafunzi wa kike wa shule za msingi na sekondari? Tuambie mambo anayofanya kwa kutoa takwimu na kulinganisha na waliomtangulia au wa nchi jirani.
4. Tumheshimu kama mama, mke wa mtu, mke wa kiongozi.Sidhani kam ndugu unayesoma hii thread na nyingine ungefurahi kuona watu wasiomfahamu mkeo, mama yako, dada yako wakimshambulia na kumponda. TUWE WASTAARABU JAMANI.
Nafikiri michango imeenda tofauti na mada ya thread hii kama nilivyosema mwanzo, hivyo ulitakiwa kuliona hilo na kuwakumbusha wana JF lakini sio kuongelea ustaarabu, furaha, heshima na mengineyo. JF sio kwa ajili ya kumfurahisha mtu. Katiba yetu inaruhusu uhuru wa kuongea bila kuvunja sheria. Sheria ipi imevunjwa hapa!
Kama kuna la maana la kumpondea liwekwe kistaarabu badala ya kuanzisha thread rejareja zisizokuwa na mantiki.