Hivi Managers wa kiume mkoje?

Sina uhakika lkn nahisi hii thread haijakamilika. Nna swali kwa huyo mdogo wako, umesema huu ni mwezi 6 sasa Manager anamtaka je huyo Manager anamtolea vitisho akiwa kazini? Pia kabla hajapata kazi je aliombwa rushwa ya ngono na huyo Manager? Je Manager anaweza kua na mahusiano na wafanyakazi walio chini yake? Hapo ni kwa ridhaa zao au wanafanya mahusiano kwa makubaliano ya upendeleo kazini. Nijibu hayo' Nachoshauri kwasasa hatakiwi kuacha kazi ila afanye uchunguzi na kuomba ushauri kwa watu anao waamini kwa mawazo yao kwa maana Takukuru lazima kuwe na ushahidi wa mtendwaji kulazimishwa kitendo icho.
 
Sasa anaanza vitisho juzi kamchorea dili la kuitwa board room halafu akamfungia kwa njee .
Isingekuwa ni wasamaria saa tatu usiku sijui ingekuwaje asingetoka
Nikodisheni mie nikajitambulishe kwa huyo Manager,hata msumbua tena Mdogo wako!!
 
Ripoti takukuru apate adabu yake
 
Dah! Yani unatoa mbinu kabisaa ya mwanaume mwezako kuteketeaaa rumande
 
Weweee acha hizo bhana bado mdogo ni 22 tu eti
22 hatongozwi ? Mtu mzima huyo, ndio maana kaajiriwa. Ingekuwa anaombwa ili apewe kazi au kupandishwa cheo.. ilo ni kosa, ila kama anatongozwa kama wegine yeye atulie na msimamo wake wa kuchomoa au akubali au akamtabulishe jamaa yake kwa huyo msela
 
Mshitakini HR.

Wafanyakazi walio chini yangu wana enjoy mahusiano mazuri sana nami. Kikazi zaidi.
 
Huu uzi watu wanaandika kama wamekatwa vichwa aisee.

Sasa takukuru inahusikaje na suala la kutongozana watu wawili na wewe kaka mtu huyo mdogowako kwani yupo shule maana umeandika as if ni mwanafunzi anayesumbuliwa na mwalimu sasa meneja akimtaka kuna kosa gani kumtaka mtu ni kosa.

Namshauri huyo meneja ambebe huyo mdogo wako mpaka ofisi za takukuru amtongozee mbele ya ofisi.
 
PCCB wakafanye nini ? Kutongoza ni haki ya kila mtu. Kuna mwanamke anafukuzia hadi miaka miwili.. mwaka wa nne ndio anakubali.. Manager kaamua kukomalia mzigo. Ingekuwa labda binti anaambiwa atoe uch.i ndio apewe kazi hiyo ni tushwa moja kwa moja..
Nashangaa kwakwel yaan mtu kutongoza ni kosa ? Mwambie aache utoto hata huko takukuru wanatongozana [emoji41]
 
wandugu kumtongoza mtu sio kosa kisheria ila kumtaka bila ridhaa yake ni sexual harassment kosa liko pale pale hata kama sio mwanafunzi
 
Kwenye nyanja ya ajira anachokifanya manager huyo ni udhalilishaji na ubaguzi mkubwa. Inatakiwa sheria iwekwe ya kuwafunga watu hawa hata miaka 20. Mtu ukisha kuwa bosi ukitoka kimapenzi na huyo mtu tayari unakua upo moral wrong maana mkiaachana tu lazima utampendelea na hata msipoachana akiharibu utamtetea. Professionalism pamoja na moral ethics zinakataa jambo hili. NI UDHALILISHAJI WA KINGONO KAMA KUBAKA. HAKUNA CONSENT HAPO MAANA ANAOGOPA.
 
Unyanyasaji kijinsia ni kosa kubwa kwa nchi za wenzetu, sema kibongo bongo bado tunachukulia poa.
 
Ni unyanyasaji wa kingono nafikiri kijinsia, ni kosa ipo katika sheria, kutongoza subordinates.

Everyday is Saturday................................😎
 
Mkomeshe. Mnyime na umpevmmiliki...halafu mwambie meneja anakutaka...[emoji38][emoji28][emoji1787]
 
Peleka.manager polisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…