Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kipindi kile ilikuwa kweli na haki kwakuwa tulikuwa na sera ya kuwahifadhi wapigania uhuru kama akina Mandela, Machel wa Msumbiji na wengineo. hiyo ilikuwa enzi ya mwalimu na utaratibu huo ulisaidia kuwamuvuzisha wenzetu kutoka sehemu moja kwenda nyingine katika harakati za ukombozi. Tulifanya kazi hiyo kama kazi ya Mungu, tunastahili kutambuliwa hivyo na mataifa tuliyoyasaidia, bahati mbaya sana tuliowasaidia ni wachache wanaotukumbuka, zaidi wametuacha nyuma sana kiuchumi ijapokuwa sisi si maskini wa mali bali maskini wa akili, wapo akina Angola, Msumbiji, South Afriaca, Namibia, Zimbabwe, Uganda, Congo nikumbusheni na wengine
Nchi kama nchi ilikuwa imeamua kufanya mahusiano na vyama vya wapigania uhuru. tulikuwa na uhusiana na PLO cha Yasser Alafat kwa mfano, tulikuwa na uhusiano na POLISARIO cha Sahara magharibi. Sasa partnership yetu na vyama hivi tulikubaliana namna ya kushirikiana na sehemu kubwa ilikuwa ni namna gani wapigania uhuru wa vyama hivi watasaidiwa. Kumbuka wakati huo akina Mandela walikuwa wanaitwa Lebels and Terrorist (waasi na Magaidi) na serikali zao. Hivyo basi hawakuruhusiwa kutoka nje ya mipaka yao. Jambo lingine la pili ambalo unpaswa kukumbuka ni serikali ya makaburu ilikuwa imewekewa vikwazo na nchi nyingi duniani. Kwa hiyo raia wa Afrika kusini hawakuruhusiwa kuingia nchi zote zilizokuwa zimeweka vikwazo. Kumbuka sio kila mtu alimjua Mandela kwa sura mwaka 1962 angeweza kukamatwa mpakani na askari yeyote na kuwekwa ndani, mpaka viongozi wa juu wakatokee waje waconfirm kuwa ni Mandela wakati ameshachezea kichapo cha mbwa mwizi.uIlikuwa kazi ya MUngu ndio..ila tulikwepaje sheria ili na leo watu wasitumie sababu hiyihiyo kuwapa wehu ambao kwa ni mashujaa..si ajabu akaja rais akawapa akina osama......
Pia itakuweje kwa raia wa Tanzania akipewa passport kwa sheria na mapenzi ya nchi nyingine je Tanzania itakwa na haki ya kumtaka arudishe yao?
Nadhani tuangalie zaidi kisheria..kuna mengi tunatajifunza km kulikuwa na makosa na wema....
Kulikuwa na mambo mengi ambayo nchi za kusini mwa Afrika zilikubaliana kwa ajili ya kusaidia ukombozi kusini mwa Afrika. Kwa Mfano nchi zote zilizokuwa mstari wa mbele ziliiwekea vikwazo South Afrika, lakini nchi za mstari wa Mbele zilikubaliana kuwa Botswana iendelee kumantain diplomatica relationship na South Africa. Uhusiano huu ulisaidia wanajeshi wetu na watu wengine maalum waliotoa support kwa wapigania uhuru walienda Botswana walipofika Botswana waliacha passport zao (Za Tanzania) na kupewa passport ya Botswana na kuingia Botswana kama Watswana. Hivyo kwenda kuipa Technical support ANC na PAC.Kipindi kile ilikuwa kweli na haki kwakuwa tulikuwa na sera ya kuwahifadhi wapigania uhuru kama akina Mandela, Machel wa Msumbiji na wengineo. hiyo ilikuwa enzi ya mwalimu na utaratibu huo ulisaidia kuwamuvuzisha wenzetu kutoka sehemu moja kwenda nyingine katika harakati za ukombozi.
Nchi kama nchi ilikuwa imeamua kufanya mahusiano na vyama vya wapigania uhuru. tulikuwa na uhusiana na PLO cha Yasser Alafat kwa mfano, tulikuwa na uhusiano na POLISARIO cha Sahara magharibi. Sasa partnership yetu na vyama hivi tulikubaliana namna ya kushirikiana na sehemu kubwa ilikuwa ni namna gani wapigania uhuru wa vyama hivi watasaidiwa. Kumbuka wakati huo akina Mandela walikuwa wanaitwa Lebels and Terrorist (waasi na Magaidi) na serikali zao. Hivyo basi hawakuruhusiwa kutoka nje ya mipaka yao. Jambo lingine la pili ambalo unpaswa kukumbuka ni serikali ya makaburu ilikuwa imewekewa vikwazo na nchi nyingi duniani. Kwa hiyo raia wa Afrika kusini hawakuruhusiwa kuingia nchi zote zilizokuwa zimeweka vikwazo. Kumbuka sio kila mtu alimjua Mandela kwa sura mwaka 1962 angeweza kukamatwa mpakani na askari yeyote na kuwekwa ndani, mpaka viongozi wa juu wakatokee waje waconfirm kuwa ni Mandela wakati ameshachezea kichapo cha mbwa mwizi.
Hivyo basi kuwafanya waweze kuingia katika nchi wanaoztaka kutembela ilikuwa lazima wapate passport ya nchi ambayo haitatiliwa mashaka raia wake kuingia (sio sawa na sasa nchi imechafuka kwa kusafirisha madawa ya kulevya). Kwa hiyo basi Mandela akapewa passport ya Tanzania, na jina la Kitanzania ili imsaidie kwenda kuonana na wapigania uhuru wenzie waliokuwa kwenye makambi katika nchi mbali mbali duniani na pia kukutana na viongozi wa nchi zingine duniani kuomba support yao. Kwa hiyo passport aliyopewa Mandela haikumaanisha amepewa uraia, alipewa kama kifaa cha kumsaidia kutoka na kuingia nchi mbali mbali ikiwemo nchi yake.
MbogelaDemokrasia ina maana pale ambapo inatumika kuleta mabadiliko chanya kwenye maisha ya Wananchi. - Zitto Kabwe (MB), Mwandiga, Kigoma (21.Dec.2013)![]()
Najaribu angalia suala la uraia wa nchi mbili na Uhalali wa akina Mandela na wenzao kutumia passport ya Tanzania na ya nchi nyingine?
Je Passpot hupewa watu wasio raia?Wenye kuelewa sana haya watuwekee mdadavuo hapa.
Nchi gani Controversial mkuu??lakini hakuna uhalali wakisheria...nilidhani kuwa Tanzania ilirekebisha sheria hata kidogo ili..kuweka huu mwanya na kupitishwa na bunge hata kwa siri.
Kwa nchi ulizotaja ni controversial sana.......Mandela ilikuwa wazi kuwa kuwa alikuwa akipigania nchi halali.Ingawa pia kuna maeneo mengine Mandela naye alifanya ugaidi.
Hii quote uliipendea nini aisee...?Democrasia si Relative bana..Democrasia ni nzuri ....na haiwezi kosa maana.Wanaokosa maana ya kuwa nayo ni jamii husika.Umaana wake ndani yake ni uleule..ila watu wanaoi abuse ndio wanapoteza maana nzima yao kuichagua..
Kwa uelewa wangu finyu sikubaliani na Uraia wa Nchi mbili kwa sababu zifuatazo:
1. Hao wanaopigiwa debe ili waweze kuwa na fursa ya kurejesha uraia wao inabidi tujue sababu zilizopelekea waukane uraiawa nchi yetu, sababu iliyo wazi ni kwamba walikimbilia maslahi yao ya kiuchumi ndio maana wakaona ni bora waukane uraia wa TZ ili wapate fursa ya kuchuma huko waliko. Sasa hii u turn ni kwa maslahi ya nani.
2. Kumbukeni tunao watanzania wenzetu tuliowapa dhamana katika utumishiwa UMMA sasa wameamua kuficha fedha zetu huko ughaibuni, sasa wakipewa uraia rasmi hamuoni kwamba ndo watatuumiza zaidi? Watafanya hivyo Kikatiba? Hamuoni hatari ya kuwa na mamluki kibao ambao watakuwa kama popo? Je mmesahau mbinu za CIA na Majasusi ya magharibi ambayo yaliwatumia watumishi mbalimbali wa mashirika yasiyo ya kiserikali kuhamisha raslimali, siri za nchi yetu chini ya miamvuli ya mashirika yao ya kidini, mashirika yasiyo ya kiserikali?
3. Sasa urafiki na mabeberu ya Kimarekani na washirika wao utatunufaisha kweli? Kama baadhi yetu ambao walipewa dhamana wamefikia hatua ya kutuletea makampuni ya kitapeli kama Richmond, Dowans, Deep Green nk huku wakiwa chini ya katiba ya uraia wa nchi moja sasa wakipewa uraia tutapona?
Tafadhali rejea kauli ya Waziri wa Ardhi kule Kapunga kwa mwekezaji wa shamba la Kapunga, Ingawa mnamlaumu Mugabe lakini kwa usalama wa nchi yetu mambo ya uraia wa nchi mbili ni hatari sana kuliko wimbo mzuri tunaoimbiwa na hao madalali wa Uraia wa nchi mbili. Tuwaangalie na kuanza kuwafuatilia kwa kina.
TAFAKARI!!!!!!!!!!!!!!!!!
Pa;estine ni controversial... tena sana.Ugaidi wao unaathiri sana watu wengine.Unatoa sadaka sana watuw asio na hatia wakiwepo watanzania.Nchi gani Controversial mkuu??
Ukumbuke wakati ule hatukuwa tunasupport nchi, Malawi wao waliamua kufungamana na nchi hivyo walikuwa na mahusiano mazuri na serikali ya ubaguzi wa rangi ya Africa Kusini. Sisi tulikuwa na uhusiano na vyama kama vyama. Tukawa na uhusiano na PLO cha wapalestina na mpaka leo tuna Ubalozi wa wapalestina hapa Tanzania na hatuna ubalozi wa Isarael, pia tukawa na uhusiano na POLISARIO kama chama cha wapigania Uhuru wa Sahara magharibi waliokuwa wanataka uhuru wao kutoka kwa Morocco.
Kuhusu sheria inawezekana kulikuwa na sheria iliyowapa mwanya, lakini ninachojua (sina uhakika sana) president wa nchi amepewa mamlaka na sheria kumgrant mtu wa nchi nyingin uraia wa Tanzania au kumfutia Mtanzania uraia wake. Hivyo presidential order mnaweza kuwapa watu kadhaa hati ya kusafiria ya nchi yenu. Kumbuka Nelsona mandela alikuwa tayari ameshachoma Passport yake ya South africa kama njia ya kuprotest.
Hii isije ikatutoa kwenye mada mkuu, tutakuja kuijadilia siku nyingine, nadhani kwa kwa leo wacha tuconcetrate kwenye uraia wa nchi mbili na Mfano wa Mandela
Watanzania wanaotaka nafasi za kuikomboa Tanzania kiuchumi na kitechnologia nao wanahitaji Passport mbili....?By the way Passport wanahitaji kushika raia....sasa km akina mandela waliruhusiwa kwanini unadhani sababu zako zina uzito kiasi hicho?Watanzania leo wanataka Katiba iruhusu wananyimwa, akina mandela waliruhusiwa tena bila kabita kuruhusu...huoni kuna sida hapa logically?
Kuna tofauti ya kutumia pasi ya nchi nyingine na kupewa uraia. Nadhani hujanielewa, kama mtu amekuwa radhi kuutupa uraia wa Tanzania na kuchukua urai say wa USA, Je unadhani anania ya kulisaidia taifa hili? Kama ameweza ku acculate capital ya kutosha aje kama investor wala sio kama raia. Wengi wa jinsi hiyo huwezi kujua orientation yao kwa sasa. Kama huelewi nisemacho tafuta Novels za Kijasusi usome uone jinsi gani USA kwa mfano inavyotake advantage ya kuwapa watu uraia wa USA na wanavyotumika kufanya ujasusi kwa manufaa ya USA. Nadhani unawakumbuka mabalozi wawili wa USA hapa walikuwa weusi kama sisi lakini kwa vile tayari wana identity ya USA wanatanguliza maslahi ya USA. Hao mnaowapigia debe wameweka maslahi ya fedha zaidi kuliko uzalendo, hivyo kwa vile hao jamaa Mabeberu wanayo pesa ya kutosha watawatumia hao watakaoonekana ni waluguru, wachaga, wanyamwezi, wajita, wakurya wapare, wakwere nk kwa maslahi ya hao mabwana wakubwa. Majuzi hapa wakati wa ujio wa Obama tuliaminishwa kwamba ujio wake ulikuwa neema, Juzi tumewasikia Halmashauri ya Ilala wakilalamika kwamba ilibidi watumie Tzs. 350M kwa ajili ya usafi wa ujiomwa Obama na fedha hizo zilikuwa kwenye mipango mingine ya maendeleo. Sasa hiyo neema iko wapi kama ujio wa mgeni tu usafinunagharimu kiasi hicho cha fedha wakati waagonjwa wetu Muhimbili wanalala chini sakafuni, watoto wetu hawana madawati ya kukalia na sasa inabidi watozwe elfu 50 ili waandikishwe darada la kwanza, Ndugu huhitaji elimu ya University kuelewa nisemacho ni suala la kutulia na kuangalia tu mambo yanavyokwenda.
Tafakari!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!