Mtumishi Wetu
JF-Expert Member
- Oct 12, 2010
- 5,712
- 1,910
Nashukuru mkuu kuliona hilo, mahakama zetu zinashushiwa hadhi siku hizi hata Majaji wanawekwa wa magumashi!!!Mahakama hawana nguvu yeyote ile kwa sababu ndio walewale ndio wapo huko, Ila Watanzania cha kufanya ni moja tu!
Tumweleze MUNGU haya yote ya kwmb tumechoka na haya Mungu wetu.
Na ni Imani tosha kabisa iko nyakati itafika na Watanzania watafurahia maisha bora lakini ni mpaka uongozi wote uliko madarakani ubwagwe chini!
Mahakama wameifanya maficho yao.
Mwisho wao waja hakika!
Ni dalili ya udhaifu na kushindwa kutatua matatizo yanayowakabili wananchi wake
Wadau nimeona tujadili hili la serikali yetu kutumia mahakama zetu kama chaka la kuficha maovu yake!!! Tuliona swala la madaktari walipoanza tuu mgomo serikali ikakimbilia mahakamani kusitisha mgomo ikidai kuwa ni batili, limekuja swala la walimu wanasema swala liko mahakamani!! Sasa tuseme mahakama zetu ni dhaifu hazina sheria kali za kuweza kudhibiti watu kukimbilia mahakamani kuweka stop order??? Je ikiwa wakipeleka kesi wakashindwa adhabu zinazotolewa ni dhaifu kiasi hawaziogopi kama vile kutolewa amri ya kutaifisha na kuuza mali za serikali hadi walipe madai ya watu??? Nawasilisha!!!
Kuna haja mkuu hata mahakama zetu kwenye katiba mpya kuwe na kipengele cha maadili mtu asipewe kazi ya Ujaji bila kufanyiwa vetting tena ipitie bungeni kuthibitishwa !!! Mtu mwenye dalili za rushwa asipitishwe kuwa hakimu hata wa mahakama ya mwanzo, wenzetu Kenya wanaendelea na zoezi hilo la kuondoa uozo kwenye judicially yao!!Kauli ya PM hii hapa: (LIWALO na LIWE)
Kweli mtu anapewa mamlaka ya kuongoza raia zaidi ya 40M halafu anadiriki kuja na kauli kama hiyo jamani tutafika?
2015 Mi ningetamani iwe baadae nione ujeuri wa ccm iko wapi!
Mihimili ya ya dola si lazima itofautishwe, mahakama inatakiwa kuwa ndio kipimo cha utawala bora yenyewe iwe check and balance, sasa inasikitisha ikigeuzwa ni njia ya kukandamiza wanyonge???Wahuni wenzao
Wadau nimeona tujadili hili la serikali yetu kutumia mahakama zetu kama chaka la kuficha maovu yake!!! Tuliona swala la madaktari walipoanza tuu mgomo serikali ikakimbilia mahakamani kusitisha mgomo ikidai kuwa ni batili, limekuja swala la walimu wanasema swala liko mahakamani!! Sasa tuseme mahakama zetu ni dhaifu hazina sheria kali za kuweza kudhibiti watu kukimbilia mahakamani kuweka stop order??? Je ikiwa wakipeleka kesi wakashindwa adhabu zinazotolewa ni dhaifu kiasi hawaziogopi kama vile kutolewa amri ya kutaifisha na kuuza mali za serikali hadi walipe madai ya watu??? Nawasilisha!!!
Ndio maana tunasema lazima katiba mpya iwe wazi kuhusu mahakama ili ipate haki yake inayostahili, kuliko kutumiwa na serikali kama tambala la kufuta uchafu wake!!!Ukiangalia kwa undani Tanzania kuna mihimili miwili - Bunge an executive. Mahakama ni mkono wa state hivyo kusema ni mhimili sion sahihi kwa sababu inawajibika kwa state!