Hivi mbona zamani tulisikia neno ma-auditor lakini neno CAG halikulisikia kabisa?

Hivi mbona zamani tulisikia neno ma-auditor lakini neno CAG halikulisikia kabisa?

SubiriJibu

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2009
Posts
1,805
Reaction score
1,876
Wakuu JF nielezeni na nifafanulieni,

Miaka kama 20 iliyopita wahasibu wa maofisini walikuwa wanaogopa sana ma-auditor. Lakini woga uliishia kwao tu.

Hatukuwa tunajadili kabisa suala la CAG na kwa kweli hicho cheo binafsi nilikuwa hata sikijui.

Hivi kumetokea nini hadi leo nchi nzima tunajadili report ya CAG kama vile ni kitu ambacho hakikuwepo huko nyuma?

Nielimisheni.
 
Atakaye kuja kukuelimisha ana kazi kubwa sana. Maana kama hukujua kuna MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI kazi kubwa ipo
 
..Ni kwasababu CAG ameundiwa sheria mpya na kupewa meno zaidi ktk kukagua matumizi na mahesabu ya serikali.

..ktk awamu ya kwanza kulikuwa na nafasi ya Government Accountant and Auditor General lakini alikuwa chini ya wizara ya fedha, na taarifa yake ilikuwa haitolewi kwa vyombo vya habari kama ilivyo sasa hivi.
 
Me sielewagi kwenye wakaguzi na wahasibu... juzi kati tumeenda kufunzwa mambo ya bank reconciliation nikamuita 'mhasibu' samahani kidogo, akanirekebisha eti mimi siyo mhasibu mimi ni 'mkaguzi'
 
Yupo miaka mingi.

Wakati nasoma miaka ya 90 tulikuwa tunaandika C&AG.

Hakuwa maarufu kiviile kwa sababu taarifa yake ilikuwa ni siri akishaikabidhi Ikulu ndo basi.

JK ndo alokuja kuanzisha kuwa taarifa ya C&AG ikishakabidhiwa Ikulu Rais anaipeleka ikajadiliwe bungeni.

Na kutokea hapo inawasilishwa bungeni ndo mana amekuwa Maarufu sasa hv
 
Na ni kwavile tu huku halmashauri wqnapewa bahasha vinginevyo madudu ni makkibwa kuliko haya tunayoambiwa! Ni mkurugenzi gani Tanzania hatoi bahasha kwa hawa ma external auditors ajr hap atwambie
 
Kabla ya uhuru wa Tanganyika ofisi hii ya CAG ilifahamika kama idara ya ukaguzi wa ndani ya Tanganyika, na kiongozi wa ofisi hiyo alitambulika kama Mkurugenzi wa Ukaguzi.

Baada ya sheria ya "Exchequer and Audit Ordinance" ya mwaka 1961 jina la taasisi hii lilibadilishwa kutoka Idara ya Ukaguzi na kuwa Idara ya Malipo na Ukaguzi (Exchequer and Audit Department), pia jina la Mkuu wa Taasisi hii lilibadilika kutoka Mkurugenzi wa Ukaguzi na hatimaye kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (Controller and Auditor General, or CAG)

Hapo awali idara hii ilikuwa haifahamiki kwa watu wengi kutokana na uadilifu wa watumishi wengi wa serikali za awamu ya kwanza na pili. Ilianza kusikika kidogo zaidi wakati wa awamu ya tatu. Zilipofika awamu za nne, tano na hii ya sita, ndiyo imekuwa "burning issue of the time" kutokana na majizi na mafisadi yaliyojazana na kujificha ndani ya CCM.
 
..Ni kwasababu CAG ameundiwa sheria mpya na kupewa meno zaidi ktk kukagua matumizi na mahesabu ya serikali.

..ktk awamu ya kwanza kulikuwa na nafasi ya Government Accountant and Auditor General lakini alikuwa chini ya wizara ya fedha, na taarifa yake ilikuwa haitolewi kwa vyombo vya habari kama ilivyo sasa hivi.
Kuwekwa public kwa taarifa ya CAG ndiyo kumefanya ofisi hiyo ifahamike.
 
Yupo miaka mingi.
Wakati nasoma miaka ya 90 tulikuwa tunaandika C&AG...

Na kwa muda mrefu idara hiyo iliongozwa na bwana mmoja toka Zanzibar alikuwa akiitwa Mohammed Aboud.
 
Enzi za ujamaa, hakukuwa na transactions za maana zaidi ya kununua chaki na syringes. Kwa hiyo madudu hayakuwepo.
Leo hii serikali na taasisi zake zinafanya transaction zaidi ya laki moja kwa mwezi ndio maana madudu yanapata fursa ya kujitokeza
 
Back
Top Bottom