Hivi Michael Jackson alikuja Tanzania na kugoma kushuka uwanja wa ndege na kusalimiana na Mzee Mwinyi kisa Tanzania hewa yake ni chafu?

Hahahaha dogo, mlipigwa kamba sana, sisi tuliokuwepo pia tulikutana na story za magangwe mitaani enzi hizo. Nakumbuka MJ alipanda Nissan Patrol toka Airport Hadi ikulu na msafara wake tuliushangilia. Kufika mitaani kila mtu na story yake tofauti. Ila ukweli jamaa alikuwa powa na picha za ikulu Mwinyi hazikuwa na dosari yoyote.
Kuna kijiweni nilikuta story eti MJ kashindwa kushuka ikulu kisa kapanda gari gumu kavunjika kiuno.
Zamani hakukuwa na vyanzo vingi vya habari kila mjanja alitunga lake na kuwaaminisha vijiweni kwamba ni kweli.
 
🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣
 
Ni kweli vyombo vya habari kwa wakati ule viliripoti taarifa hiyo kuwa jamaa kasema kuna harufu mbaya.

Ila alishuka Airport na kufikia KILIMANJARO HOTEL ( enzi hizo ) na katika ziara hiyo alionana na rais wa wakati ule ( rip Ally Hassan Mwinyi ) kama kwenye picha inavyoonesha.

Lkn inaelezwa HAKUWA NA FURAHA, ila alipopelekwa kwa watoto wenye mtindio wa UBONGO SINZA huko alionesha kufurahi nao na kuimba nao nyimbo.

Pia alipanga kwenda kutembelea mbuga za wanyama SERENGETI lkn aliahirisha safari hiyo baada ya kujulishwa kuwa atatumia ndege yake kubwa mpaka uwanja wa ndege KIA. kisha atapanda ndege ndogo mpaka MBUGANI hapo AKAGOMA.

NA kuahirisha ziara nzima ya Mbugani na kuamua KUONDOKA .NA ndipo alipotoa kauli ya harufu mbaya.
 
duh umetisha kwa taarifa hii ya kina
 
dogo hongera kwa udadisi

ni hivi

wakati MJ amefika bongo ilikuwa ni siku kubwa na ya furaha sana kwa nchi yetu

maana ilikuwa ni mara ya kwanza kwa mtu huyo ambaye kwa wakati ule alikuwa mwanamuziki mashuhuri zaidi wa ngazi ya kidunia kuwahi kufika bongo

alipokewa kwa heshima kubwa kama hizi unazoziona kwa viongozi wakubwa wanapokuja kutoka huko nchi za ng'ambo

ujio wake ulirushwa mubashara (live) kwa matangazo ya radio ya taifa (hii tbc ya sasa wakati huo ikiitwa redio tanzania). maana yake yalisikika katika miji yote mikubwa na midogo, vitongoji na vijiji yaani kule kote ambako masafa ya radio hiyo yaliweza kufika. TV zilikuwa bado ila ni wazi kama zingekuwepo basi tukio hilo lingerushwa kwa watz mubashara.

alipokewa na aliyekuwa rais wa wakati huo huyu rais mwinyi marehemu, mungu amrehemu.

macho na masikio ya mamia ya watzania na serikali yao kwa ujumla kwa wakati ule yalikuwa kwa msafara wa mheshimiwa MJ.

hayo uliyoambiwa kuhusu MJ kushika pua ni ya kweli sio uongo. Mara baada ya kushuka kwenye ndege MJ alionekana kupata shida na hewa ya bongo na mara nyingi alionekana akiiminyaminya pua yake kuashiria pengine alikuwa akipata hewani ambayo haikuwa sawa kwake. hali hii kwa kiasi ilizua maswali kama unavyoweza kutegemea hata ingetokea leo hii.

kuhusu kwanini MJ alikuwa anaminyaminya au kushikashika pua. Je hewa ilikuwa si rafiki au ilikuwaje hiyo kila mmoja atabaki kuwa na tafsiri yake lakini ukweli anaujua yeye mwenyewe MJ na mungu wake.

kwa uchache hali ilikuwa hivyo.

karibu.
 
haha hiyo ya kuvunjika kiuno wana wa kijiwe walitisha hahah kifupi enzi hizo nadhani kulikuwa na wajanja wachache wa vijiwe wazee wa fiksi ilimradi tu kijiwe kinoge watatunga yaoπŸ˜‚πŸ˜‚
 
umetisha sana....au labda alikua anashika shika pua kwa sababu ya plastic surgery alokuwa akifanya??πŸ˜‚
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ bongo nyoso
 
Harufu ya amonia na phosphorous.Ni harufu maalum za maeneo ya bahari na wala sio mbayo.
Watu wa kuja Dar ndio huwa wanaisikia kwa mara ya mwanzo wanaona ni mbaya.
hata mimi ilikua inanisumbua miaka nakuja Dar kusoma
 
Tazama video ya earth song ya mj utajua kuhusu uko kaskazi mwa tanzania na mj
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…