Hivi Millage ina matter?

Mhh wabongo sio watu
 
Hahahahaha kinachonishangaza ndio habari ya mjini kama ist....halafu yanabugia balaa
Crown Japan inatumika kama Taxi au gari za PolisPolisI (Patrol) ila Bongo mtu kavimba utadhani kanunua gari ya maana.
 
Kwangu mie gari lenye milage nyingi , ndio chaguo langu kama unaanunua used
Gari lenye milage nyingi ni kielelezo kimoja kuwa lilitunzwa na kufatiliwa vizuri katika maisha yake .,

Kuna jamaa youtube ana scania 142 , imetembea km milioni 4.1, na bado gari ipo poa
 
Ungetaja km ingependeza zaidi unadhani kila aliyoko humu anajua Dar- chalinze ni umbali gani?
 
Inaweza kuwa viceversa.

Gari yenye mileage ndogo unaweza ikawa imetunzwa zaidi pia.

Kuna watu wana mpaka magari matatu nyumbani na wanatumia usafiri wa ofisi.

Unadhani hizo gari zitakuwa na mileage kubwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili swali halina jibu 'General' na kuna divided opinions kwa sababu kila mtu ana experience tofauti. Suala la kma mileage kujibiwa lazima u-narrow down to aina ya gari, aina ya engine, historia ya maintenance, driving conditions gari limepitia etc.

Mfano, kuna Toyota au Lexus zina 300,000km kwny odometer zipo barabarani zinatembea na kuna Toyota zina 50,000km na zimelala garage zina mauza uza kila kona. We utanunua ipi? Hata mim sijui kwa sababu kuangalia uzima wa gari kwa mileage pekee haitoshi.

Ukiongelea Engine tu specifically, zote huwa zina lifespan inayopimwa na mileage endapo tu vigezo na masharti yamezingatiwa e.g. Routine Maintenance etc. Mileage nyingi ni kiashiria kuwa gari imetembea sana ila imetunzwa na engine ni imara na inatimiza ahadi ya umadhubuti wake.

Ushauri wangu, mileage is both good and bad depending na type ya gari, engine, etc. Be an informed consumer, kma unataka kununua gari used lazma uchukue your time kustudy gari yako hata online tu usome, its free resource zipo kibao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana mkuu kwahiyo ww vigezo vyako vyakununua gari ni millage?? Kama ndio hivyo pole sana aisee.hizo nyingi zinashushwa .njoo kwangu ukitaka nitakushushia hata isome 10 au 100 au hata sifuri ni ww tuu k kwangu u
 
isn't there any way to restore the mileage to zero?!
Yes boss inawezekana kabisa karibu sana kama unashida hiyo ni kazi ya nusu saa au dk 15 tuu..

Msinunue gari kwa kuangalia millage acheni kabisaaa aisee..

Kama unashida yakushushiwa millage well come JO AUTO TECH tupo mwenge karibu na chuo cha kilimanjaro mita chache kutoka msikiti mkubwa wa mwenge..
 
WISDOM, WISDOM, WISDOM

Ukinunua gari kwenye Yard za bongo mfano IST yenye mileage ya km 20000 itaanzq kusumbua mapema kuliko mtu aliyeagiza IST Japan yenye mileage mathalani km 80000... endapo wamiliki wote wawili utunzaji wao unafanana...

Why..?
Wabongo wengi si waaminifu...
Kuna uwezekano mkubwa sana wafanya biashara wanaagiza magari ambayo ni above km 120,000 kwa bei chee....yakifika bongo yanashushwa Milage yanasoma mfano km 20000, 30000 na mengi hayazidi km 50000.. kisha wale wazee wa kununua gari kwa kuangalia mileage wanaingia kichwa kichwa wanapigwa...

Kwa mimi msimamo wangu bora niagize gari Japan lenye mileage ya km 150000 kuliko kununua yard za bongo gari lenye km 40000.

Nina mfano hai...nina gari niliagiza Japan likiwa na Km 110,000 na sasa lina km 150000+...the car is still running very smoothly ninaijali service, no any leakage..gari ni Nissan namba C...Nina mtumish mwenzangu ana IST namba C inasoma Km 70000....inamsumbua kila idara...yaani ni majanga...akifungua kwenye hood unamwonea huruma..Imenunuliwa hapa hapa bongo...inamsumbua si bearings, si exhaust system inalia kqma subaru anaambia mafla i ekufa, leakage za hapa na pale....mbaya zaidi imegongwa ikanyooshwa nikimwambia hivyo anabisha..

Mbaya kuliko hii IST mvua ikinyesha maji yanajaa pale kwenye sehemu ya kuweka spare tire pako kama karai flani hivi..yanaingilia wapi...hatujui..?
Nilimshauri auze aongezee pesa anunue gani nyingine..

Wisdom, wisdom , wisdom.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…