Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,809
- 15,421
Niko hapa maeneo ya Mlimani City na mfanyakazi mwenzangu ambaye bado hajaoa
Tumesimama mahali ambapo kila anayeingia na kutoka hapa Mlimani City tunamuona.................. Kuna mabinti wengi wazuri wa kuvutia wakiwa na vivazi ambavyo ukiwaangalia.............Mashaaallah, wamejaaliwa hasa........ Wenye Pedo haya wenye Skin Jinzi haya, wenye Suruwale za kubana makalioni tena mlegezo wakiwa vitovu nje nao wapo, wenye Vikuku haya wenye Viatu vya Makhirikhiri twende kazi, ili mradi kila mmoja kapendeza kama mamtoni mwanawane..................
Yule mwenzangu nilipomuangalia namuona kawakodolea macho huku domo limemlegea utadhani fisi aliyeona mnofu...............
Namuuliza, Mwenzangu kulikoni umetoa macho kiasi hicho?
Aisee..... Kweli Mungu anajua kuumba, mabinti wazuri namna hii, hivi mimi nitatosheka na mwanamke mmoja kweli....................! Alinijibu huku akiendelea kuwakodolea macho.........
Mh! Nilibaki kuguna..............