Hivi mkeo huwa anachukulia vipi unapokuwa katika kipindi kigumu cha kukosa fedha?


Sijajua.
 
Mume mtamu jamani.

Akiwa na stress mliwaze na msaidie majukumu yake pale unapoweza.

Mpe hope kwamba mambo yatakaa Sawa tu.

Believe in him, pray for him.
Mke wangu yuko na hii tabia kama hatabadilika hapo baadae
 
Pesa ni sabuni ya roho kibao chake Aziz Abdi na Orchestra Benga Africa
hapo inabidi uvumilie kununiwa
 
saa zingine wamama inabidi waelewe utafutaji mgumu unahitaji maombi na uvumilivu siyo kutukalia kooni kama sisi ni wahaini sana
pesa siyo mkodombwe kwamba kila mtu anayo ipo tofauti jama
 
Sio mke ila ni mchumba, nilikwama kidgo kwenye biashara zangu japo ni ndogo bado nipata loss, alinipa kiasi cha fedha na wala ajanidai hadi sasa yapata miezi minne N.B pesa alizonisaidia ni ndogo mnoo kulinganisha ambazo mimi nimempatia.
yani kama mkeka bana 🤣 🤣
 
Tatizo la kina mama wengi pesa ya mme ni yenu wote, na ya mke ni yake mwenyewe na hapo ndio uchungu unaanzia 🤣 🤣 🤣
 
Pole sana, huyo sio mke, na sio kila mwanamke ni mke, mke ni yule ambae mnasimama pamoja katika vipindi vyote vya maisha bila kujali, ndio maana hata kiapo cha ndo kinasema wazi kwamba mtakua pamoja kwa shida na raha, magonjwa dhiki na tabu

Ukiona mwanamke hawezi kuheshimu hayo maneno ya kiapo cha ndo basi hapo umepigwa pakubwaa
 
Mwanamke naye anatakiwa awe na balance ya mahitaji yake madogomadogo na siyo kulialia njaa tu kila wakati.
 
Ndicho kipindi mwanaume huwa anatakiwa kuchaguwa katika mambo matatu ili kunusuru maisha yake.

1/ achaguwe kuvumilia mateso na dhihaka za mkewe ili akifa aende mbinguni Kwa uvumilivu alioufanya.

2/aamue kuwa na mchepuko ili ndoa iweze kudumu.

3/aamue kuachana na mkewe ili kulinda heshima yake.

Hii ikikutokea ukiwa na umri chini ya 35 huwezi kuelewa, ila ikikukuta ukiwa na umri wa zaidi ya miaka 45 ndipo utaelewa kwa nini wanaume hufa haraka kuliko wanawake kwenye ndoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…