Hivi mkoje nyie?...!

...duuuuuh, ha ha ha...VC huyo ana hila,...anaye anayemchekesha akiwa nje ya nyumba 😀

Mi nadhani njia nzuri ni kusemezana... mwanaume ukiona mkeo kanuna..muulize kwa upole tu... usijifanye kichwa ngumu ..uondoke kwenda kwenye kinwaji na kujichekesha kwa mabaamedi.Ukifanya hivyo unaongeza tension..na ukizoea hivyo kumtia simanzi mkeo ujue shida hujiandika usoni.Mkeo atapata wa kumchekesha na yeye.Siku hizi kuna technolojia...mobile phones, internet kama hivi... hivyo basi bora ku minimise risks!
Ukiona humtaki bora umwache mapemaaa!
 

...kuachana sio suluhisho VC, kila ajaye atakuja na package yake.
Utaachana na wangapi?
 
 

...ukimuuliza atakujibu kwamba hajanuna 😕
 
Nimefuatilia kwa karibu hii Mada, binafsi sina imani kwa asilimia Mia moja ushauri wa kumtoa "out" au "kumfanyia jambo jema" mwanamke anayonuna every time pasipo sababu" labda kama unajua chanzo chake ni nini.

Wajuzi wanasema maisha ya ndoa yametawaliwa na usanii kuliko fani nyingine yeyote duniani, na hata asiejua "kupaform" kwenye jukwaa, katika ndoa anaweza kuigiza ukashanga!...Unapogombana na mkeo akakununia mara nyingi kama anakujali au kukuogopa anakuwa amekununia chumbani tu lakini akiwa nje na mbele za watu atajichekeshachekesha na pengine hata huko chumbani utapumzika nae "same bed" kwa staili ya Mzungu4 au atizame "wrong sight". Usniii unakuja pale kama alitaka kwenda bafuni nawe ukiwa na mwelekeo huo huo wa bafu, ataghairi labda aende kwenye "dressing table" hata kama hana shughuli hapo au ajifanye anatoka nje,......au vipi atajifanya anatuma sms nk.


Unaweza kukutamzee anamdunda mama kila kukicha lakini kwa usanii, mama analilia chumbani na pengine akiulizwa anaweza kutoa ushuhuda tofauti na hali halisi! Mengi mnayasikia kwenye maharusi wapo wazee wanaoshuhudia uwongo kwa kueleza hawajawahi kukwaruzania tokea waoane!!! (Uongo mtupu!, na sijui kama wapo wanandoa wataweza kuikwepa dhambi ya "kusema uoongo").

Pengine ukiwa na mtoto mdogo makali ya ugomvi huwa yanapungua.....

Wazoefu wa masuala ya familia wanasema watoto wanasaidia sana kupunguza makali kwenye ugomvi wa baba na mama kwani mara nyingi wazazi wakiwa na jazba zinazotokana na wao wenyewe, siku zote mmoja kati yao atajifanya kupuuza pale anapokuwepo mtoto aidha kwa kuogopa mtoto asisikie au kwa kujaribu kuonyesha mbele ya mtoto kuwa yeye hana hatia pengine kwa kumtaka mtoto amwone yeye ni bora kuliko na mwenye mapenzi ya kweli kwa mtoto.


Mama akiwa "maza hausi" pengine kununa kunapungua, lazima atakusemesha tu kama hujaacha chochote home na unataka kuondoka labda awe na kiburi za kuzaliwa atakuchunia lakini vyvyote, mtawasiliana tu haka kwa sms ya kukukumbusha au kukulaumu kwa kutojali familia!.............
 

Mkuu, PMS doesnt haichukui mwezi mzima, na juhudi zako si za mara moja ni muendelezo

As VC said probe zaidi na zaidi, ila pia uelewe yeye ni binadamu, na anaweza akawa na emotional contacts outside hiyo nyumba yako

Maka ningekuwa wewe i would have gone further in probing ili kuapata haklika ya way forward!!! Kwa kawaida mtu hawezi kununa miezi, unless kuna tatizo kubwa zaidi

Pia waweza jisifia kilimo kwanza lakini kati yenu kukawa hakuna communication... hapo unatwanga maji kwenye kinu!!! BTW, how can you have kilimo kwanza kwa mtu aliyenuna???😛 hapo sikubaliani na wewe asilani!!! Kilimo kwanza kinaendana na maandalizi [kama nilivyosema mwazo], sasa hayo maandalizi bubu!!!???

Hebu jaribu basi for 3 weeks mazee??!!
 
Mpeti mpeti huyo Mbu, muda mwingine huwa tunanuna kwa kutaka attention tu. Hebu msikilize kwanza anahitaji nn, labda anataka bembelezo lako huyo.
 
hawa watu wanamatatizo mkuu, siku zote anajua kununa ndio suluhisho la tatizo lake, na anajua tu kuwa lazima utamuuliza una tatizo gani atakidai bado kuendelea kununa hadi umbembeleze. Hapo utakuta anataka kitu sasa anajua akikuambia kavu kavu unaweza kumtolea nje, ndio maana anaununa ili umuulize kwa kumbembeleza halafu ndio atasema. kama ningekua mimi nami nauchuna kinoma noma
 

Ah shemeji mie tena? wala sidongoi pale penye ukweli ati. Ninakubaliana nawe kuwa kina mama wengi tuna tabia hii ila kama alivyosema dada Vera huwa kuna sababu behind yaani dada kuna ujumbe anataka kukufikishia but ndo hatujui njia sahihi!

Ila seriously kuna wanaume wanaonuna na usiombe ukakutana naye loh! Utajuta. Mie wangu alikuwa ananuna bila sababu asubuhi hadi usiku akirudi ni kuchuna tu hadi unachoka halafu nite kali ghafla bin vuu unasikia kono linateremshwa hazina!! Sijui wakoje wa namna hii!
 
maudhi ni sehemu ya maisha katika ndoa na hayo ndo yanaongeza tamu ya penzi
anaweza akawa amenuna cause umeingia huonyeshi care yoyote unajifanya kuchoka na kazi ....na yeye amekumiss kumbe weye unajidai busy na JF na TV
 


ndo maanake!akinuna wewe unajichoma sindano ya ganzi.ukiona vipi haeleweki unaki-hold CHAKULA CHA USIKU!
 

mie kwa kweli nakerekaga sana na hiyo tabia ya kununia ndani bila kueleweka tatizo, mie kwa upande wangu huwa cmchunii bila kumweleza tatizo, nina frnd wangu yeye mr wake ni kuuchuna always, na yeye hamuulizi hili wala lile kama kuna tatizo/maelezo ni ku2miana msg tena wakiwa maofcn sasa namuuliza mtaendelea na hii hali mpaka lini, frnd anasema ameshambembeleza/muomba aiache hiyo tabia lakini mr ndio kwanza anaiongeza kwa solution ni kuchuniana tu.
 


sasa Mbu hapo unatakaje, hata kama ni saa 5 za ucku na hatujawacliana kwa lolote yani cjui upo kona gani niculize?
 
sasa Mbu hapo unatakaje, hata kama ni saa 5 za ucku na hatujawacliana kwa lolote yani cjui upo kona gani niculize?

Dada we acha tu hawa wana mambo halafu usipouliza ataona hujali na ukiuliza hakujibu mie hata huwa siwaelewegi hawa viumbe
 


Hivi weye robbot kweli una nafasi ya kukaa na mywife wako kweli, maana muda wote unabofya, au nae ulimpata hapo hapo "jeiefu, na hivyo yuko hapo pembeni!.......te..he..te..!
 
Dada we acha tu hawa wana mambo halafu usipouliza ataona hujali na ukiuliza hakujibu mie hata huwa siwaelewegi hawa viumbe


mie kuuliza ni muhimu labda uwe mwenyewe umeshaniambia mizunguko yako na ndio ukereke vizuri kama anakereka, sasa mie nitajuaje jamani kama umepata tatizo huko? hawa viumbe hawana tafcr ya kutosheleza kabisa mami.
 
mie kuuliza ni muhimu labda uwe mwenyewe umeshaniambia mizunguko yako na ndio ukereke vizuri kama anakereka, sasa mie nitajuaje jamani kama umepata tatizo huko? hawa viumbe hawana tafcr ya kutosheleza kabisa mami.

Hii huwa haipo kwenye tafsiri yao wao ukiuliza anahisi unamlilia wivu ah!!
 
Haka ka tabia hata wanaume kibao wanako japo ni ya kike zaidi.Kuna story huwa naisikia kuwa mtu na mkewe walikuwa wamenuniana siku kadhaa .Mume akapata safari ya nje ghafla na inabidi aondoke na ndege saa 11.alipofika nyumbani ikabidi amwandikie kimeseji mkewe kwenye karatasi kuwa amwamshe kabla ya saa 11 ili wahi.Na mkewe ilipofika muda na yeye akamwandikia kimeseji kuwa muda ushafika ajitayarishe.Sasa baba kuja kuamka saa 11 ishapita na keshachelewa akaanza kumkaripia mkewe kwa nini hakumwamsha.Hapo kilichobakia ugomvi na majuto.Yote hayo ni hasara ya kununa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…