MwananchiOG
JF-Expert Member
- Apr 4, 2023
- 1,970
- 4,037
Inashangaza sana baadhi ya mashabiki wa Simba kutupa lawama kwa mwamuzi wa mchezo wengine wakitoa lawama kwa serikali, Swali la msingi ambalo wanajisahaulisha, Hivi kweli walikuwa serious wakitarajia kuifunga Young africans?
Wanapaswa kushukuru mbinu aliyoingia nayo kocha wa Yanga (kuamua kuwaheshimu) , uchovu baada ya mechi za Afcon na hali ya uwanja na mvua zilizomzuia Young africans kucheza mchezo wao waliouzoea!
Hakuna timu ya shirikisho inaweza kufua dafu kwa timu hata zilizopo pot 4 club bingwa! Achilia mbali pot 2&1. Kuna timu ya shirikisho anaweza kuifunga pyramids ya Mayele? achilia mbali hao kina orlando pirates, MC algiers, CR Belouizdad, ES Tunis, Raja CA, Mamelodi, Al ahly nk.
Ifike wakati heshima ichukue mkondo wake! Ukiangalia kikosi cha Young Africans ukilinganisha na wapinzani ni kama watoto wa shule ya msingi wanaenda kucheza na wanaume kamili na matured wa Young africans.
Hivi kweli unamlinganisha Balua na Mzize, Dube, Aziz ki, Baleke? Hata physiq tu wakikaa pamoja unaona tofauti. Sijui vitoto kama Ahoua ambao bado wanajitafuta, Ateba,sijui Mutale ndiyo striker tegemezi mbele ya makipa matured na experienced kama Diarra? huko si kuwatafutia lawama! mbele ya mabeki kama Dickson job, Bacca ambao kina shalulile hawakuweza kuwafunga?
Timu kikosi cha kwanza beki Hamza na midfield Kagoma alafu uwachezeshe na watu matured na experienced kama Aucho? Maxi? Pacome?
Kama sio mbinu za mwalimu wa Young Africans kuamua kuwaheshimu bila kufunguka (ambapo alikuja kugundua kipindi cha pili baada ya kuona hamna haja ya kuwaheshimu maana hakuna kitu) na kama uwanja ungekuwa kwenye ubora, huenda tungezungumzia magoli mengi sana.