Hivi Mnajua Kocha wa Zambia Herve Renard aliomba Kuifundisha Taifa Stars - TFF Wakamkataa!!!

Wachezaji ndiyo wa kulaumiwa na siyo kocha. Tujiulize mara ya mwisho kushiriki AFCON hadi leo ni makocha wangapi tumekuwa nao na hakuna lolote la maana, je wote hao hawana mbinu za ufundishaji? Ni muda muafaka kuiweka hii timu ya wazee pembeni na kuishirikisha timu ya chipukizi.
 
Usimba na uyanga unachangia sana kuua soka la tz

Ulipaswa kusema Usimba na Uyanga ndio kiini cha mpira wetu kudidimia. Hizi timu zote hushinda kwa kubebwa (kama magamba wanavyobebwa na "tume ya uchaguzi").
Usipokubali fair competition na ukategemea kubebwa utapata "mafanikio" ya ndani lakini ujinga wako utajidhihirisha wazi siku utashindanishwa na mwingine anaetoka mazingira tofauti na kubebwa. Yanga na Simba zisimamishwe kushiriki ligi angalau kwa miaka 3 ili mentality ya Usimba na Uyanga uishe!
 
nadhani tatizo letu sio kocha ni wachezaji wenye vipaji ni wachache au ni wale wale hawana jipya,hakuna ushindani wa kuchezea TAIFA STARS, Wacheza wana motisha ndogo,washabiki pia tunamatatizo tunacheza mpira majukwani hatuna uhalisia!timu zetu hazifanyi vizuri kimataifa!hata kocha mzuri kiasi gani apewe Taifa Stars tusitegemea suluhisho la ushindi!tubadilishe mfumo wetu wa mpira!wadhamini wajitokeze,mpira uchezwe mikoani,ligi ziwe za ushindani,waamuzi watende haki na makocha wawe professionals
 

BT................ naomba nikuweke sawa. ...................

hapo kwenye red, wakati ule kulikuwa na FC na sio KK ikulu ya zambia..................

kwenye blue, ............... hawakujitoa mashindano ya kimataifa ila waliomba kama wiki mbili hivi kuteua timu nyingine na baada ya kuiteua timu mpya............ ilicheza mechi zote zilizokuwa zimebaki kikamilifu na kufaniukiwa kufuzu kucheza fainali za AFCON mwaka 1994 ................ na huko kwenye fainali, .............iliweza kuingia fainali na bafanabafana ............. wakati faianali hizo zilizofanyika kwa mara ya kwanza south africa................ ikishuhudiwa na madiba nwenyewe live.................
 
Hata tungemchukua morinyo au ancellot......bado tusingepata mafanikio...tatizo waswahili hatuelewi..kocha si sababu
 
Kichwa cha mwendawazimu kila mtu anasubiri ziote afanye mazoezi.
 

uko sahihi. Hakuna kitu ambacho tuko serious nacho hata kimoja. Wazembe wavivu na si mpira tu. Hata maofisini.
 
Tatizo la Tanzania wanadhani kuwa kocha kuwa mzungu ndio kufanikiwa....ona sasa wenzetu Zambia wamechukua kombe sisi bado tunauza sura nahuyu mzungu.
 

Ahsante sana Dr, kiwango cha Wachezaji wetu wa sasa huwezi kabisa kukilinganinisha na enzi za akina Maulid Dilunga, King Kibaden, Kitwana Manara, Omar Kapera, Hassan Gobbos, Willy Mwaijibe au akina Sunday Manara, Mohamed Salim, Mohamed Chuma na wengineo wengi. Hata tupate kocha mzuri kiasi gani hatuwezi kufika kokote kwa sababu kiwango cha wachezaji wetu kwa sasa ni kidogo mno ukilinganisha na miaka ya nyuma.
 

Inshu zima ni malipo, kama smart guy anayeweza kuziona zile vectors za speed kati ya upepo na mpira akisikia wanalipwa vizuri na mfumo unashawishi vizuri kuachana na madude mengine, kwa nini asifanye bidii kupiga soka? Na kwa nini wazazi wasimruhusu mtoto wao mwenye kipaji cha soka kufanya vitu vya mpira na si kukomaa naye na udaktari au uhandisi au uanasheria?

kwa hiyo hapa ni inshu nzima za malipo, mfumo wetu wa kubebana bebana bila kujali uwezo nawatu kutoamini kuwa kama watoto wao watawaruhusu kucheza mpira, wanadhani wataharibikiwa. kwa hiyo bado kuna mentality za hivyo!!!
 
Chibingo, tatizo la Watanzania wanaoongoza soka katika TFF na katika vilabu vyetu wengi wao huwa ni wanasiasa tuu. Hugombania nafasi hizo ili wajulikane na baadaye utawasikia wanagombea UBUNGE.
 
Tatizo laTanzania sio kocha bali mfumo tulio nao sio wakutengeneza teaminayoweza kuleta ushindani kokote mfumo wetu unaruhusu wahuni kuingia katika team kubwa na hatimae taifa sasa leo Bongo hata akija Mourinho bado tutakuwa kichwa cha mwendawazimu

Na huo mfumo wa TFF unaakisi mfumo mbovu uliopo Serikalini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…