hivi mtihani wa taifa form 6 watatumia grade zipi?

TRamadhani

Member
Joined
May 30, 2013
Posts
48
Reaction score
18
Wizara imedhamiria
kufanya harmonization ya masuala ya
alama katika mitihani ya Kidato cha
Nne na Kidato cha Sita ili kupata
muundo mmoja na ulio wazi kwa
wadau wote wa elimu ya sekondari. Lakini pia serikali imedhamiria
kuhakikisha tathmini za wanafunzi
katika ngazi mbalimbali zinakwenda
sambamba na matarajio ya mitaala
inayotumika na ambayo inahuishwa
mara kwa mara ili iendane na wakati na mahitaji ya elimu katika ngazi
mbalimbali. VIWANGO NA UTARATIBU KUANZIA
MWAKA 2013 KWA KIDATO CHA NNE
NA KIDATO CHA SITA KWA MWAKA
2014 Baada ya kufanya tathmini ya maoni
mbalimbali ya wadau, misingi ifuatayo
ilizingatiwa katika maamuzi kuhusu
makundi ya alama na muachano
wake: a) Alama zitakazotumika zitakuwa A,
B, C, D, E na F. Muachano wa alama kati
ya kundi moja hadi jingine utafanana,
isipokuwa tu pale ambapo itaonekana
kuna sababu na hakuna athari za
kuwa na muachano tofauti na ule ambao umetumika katika makundi
mengine. b) Makundi ya alama hayatakuwa na
clusters isipokuwa pale ambapo
itaonekana kufanya hivyo kunaleta
tija katika kupata picha ya wahitimu
kwa ajili ya matumizi mbalimbali. Kwa
mantiki hii (i) makundi ya alama A, C, D, E na F
yabaki na cluster moja moja bali kundi
la alama B litakuwa na clusters mbili.
Kundi la kwanza litakuwa la wale
ambao wamepata alama kati ya 50
mpaka 59 na litaitwa B na lingine litakuwa la wale ambao wamevuka
uwigo wa 50 hadi 59 na kuelekea
uwigo wa 60 hadi 74 na hili litaitwa B+
(angalia jedwali hapo chini). (ii) Pamoja na kuwa na muachano wa
alama 26 kama jedwali linavyoonesha
hapo chini, alama A kwa miaka mingi
imekuwa ikianzia alama 75 hadi 100
na kwamba pamoja na uwigo huo
bado wanaofaulu kwa kiwango hicho ni wachache sana. Kwa mantiki hii,
hakuna haja ya kubadilisha uwigo ila
juhudi ziendelee katika ufundishaji na
ujifunzaji ili kiwango cha ufaulu
kiongezeke na kupata wanafunzi
wengi zaidi wanaofaulu katika kundi hili. (iii) Pia, pamoja na kuwa na muachano
wa alama 20 kama jedwali
linavyoonesha hapo chini kwa miaka
mingi, huko shuleni mwanafunzi
aliyepata alama 21 na hadi 30
alihesabiwa kuwa na ufaulu wa chini kabisa au hafifu kwa kiwango cha
alama D na ingawa ilikubalika ufaulu
wa aina hiyo kwa mazingira ya nchi
yetu unaridhisha. Alama Filikuwa ni
kwa wale waliopata chini ya hapo.
Hivyo, alama F itaendelea kuwepo na itaanzia alama 0 hadi 19 na E itaanzia
alama 20 hadi 29 na D – 30 -39. Lengo
la muundo huu ni kuwa alama
mbalimbali, isipokuwa kwa makundi
machache, zianzie kwenye 0 yaani 0,
10, 20, 30, 40 na kuendelea badala ya kuanzia kwenye moja yaani 1, 11, 21,
31, 41 na kuendelea. Hii ni kwa ajili ya
kuleta mtizamo unaofanana katika
ngazi mbalimbali za elimu ambapo
kwa sasa ngazi ambazo siyo za elimu
msingi na sekondari zinatumia muundo wa kuanzia kwenye 0 badala
ya 1. c) Uwigo wa jumla wa alama kwa
Kidato cha Nne na Kidato cha Sita
utaendelea kuwa wa alama 0 hadi
100 na kila kundi katika uwigo huu
limepewa tafsiri kwa ajili ya kuamua
mambo mbalimbali yanayohusu maendeleo ya mwanafunzi kulingana
na malengo ya mtihani husika.
Kimsingi, tafsiri zifuatazo zitakatumika (i) Alama A itakuwa na maana ya
ufaulu uliojipambanua (distincion or
outstanding performance), (ii) Alama B+ itakuwa na maana ya
ufaulu bora sana (excellent
performance), (iii) Alama B itakuwa na maana ya
ufaulu mzuri sana ( very good
perfomance), (iv) Alama C itakuwa na maana ya
ufaulu mzuri (good performance); (v) Alama D itakuwa na maana ya
ufaulu wa wastani (low performance), (vi) Alama E itakuwa na maana ya
ufaulu hafifu (very low performance),
na (vii) Alama F itakuwa na maana ya
ufaulu usioridhisha (unsatisfactory
performance). Wataalamu katika maeneo mbalimbali
ya elimu na ulimwengu wa kazi, kwa
kushirikiana na Wizara, watatoa
maana ya tafsiri hizi kiutendaji katika
maeneo yao kulingana pia na mahitaji
yao. d) Alama C iwe ndiyo alama ya ufaulu
mzuri ambao hauhitaji urekebu wa
lazima, wakati alama D na E ni alama za
ufaulu unaohitaji urekebu kadri
mwanafunzi atakavyokuwa
anaendelea na masomo ili kuthibitisha kama mlengwa anaweza na kulingana
na mahitaji ya eneo husika (targeted
remediation). Alama F iwe alama ya
eneo linalohitaji urekebu wa hali ya
juu (intesive remediation) ili
mwanafunzi huyo aweze kumudu masomo kadri anavyoendelea kukua
kielimu ama atakapoingia katika
ulimwengu wa kazi. e) Makundi ya alama yatajumuisha CA
kwa kiwango cha asilimia isiyozidi 40
na mtihani wa mwisho kwa asilimia
isiyozidi 60 kwa makundi yote ya
watahiniwa ikiwemo wale wa
kujitegemea (private candidates). Hii ni kwa kuzingatia kwamba CA siyo vizuri
izidi uwigo wa alama ya ufaulu mzuri
unapoanzia ambayo ni C au 40. f) CA kwa upande wa Kidato cha Nne
zitokane na mtihani wa Kidato cha Pili
(alama 15), matokeo ya Kidato cha
Tatu (alama 5 kwa kila muhula, na
hivyo jumla ya alama 10), mtihani wa
Mock (alama 10) na kazi mradi au Projects (alama 5). Kwa upande wa
Kidato cha Sita, CA iendelee kutokana
na muundo unaotumika sasa. g) CA zitumike pia kwa watahiniwa wa
kujitegemea. Kwa upande wa
watahiniwa wa kujitegmea ambao
wanarudia Mitihani, CA zao zitumike
zile zilizotumika kutoa matokeo yake
ya mitihani ya awali. Kwa watahiniwa wa kujitegemea waliopitia mfumo wa
Qualifying Test (QT), matokeo ya QT
yatumike kama CA na mtihani wa
mwisho uchangie alama 60. h) Kwa vile alama endelevu kwa
mwaka 2013 kwa wanafunzi wa
Kidato cha Nne tayari zimeshawasilish
wa Baraza la Mitihani Tanzania, alama
hizo zichangie asilimia 40 katika
mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2013. i) Muundo wa wastani wa alama
katika ufaulu (Grade Points Average
ama GPA) utaandaliwa na kuanza
kutumika pale utakapokuwa tayari na
wadau wataelimishwa kuhusu
muundo huo ili wapate kuufahamu na manufaa yake katika elimu ya
sekondari. j) Muundo huu mpya wa alama
utatumika kwa mzunguko wa miaka
minne kabla haujahuishwa tena ili
kuupa muda wa kutosha kuona aina
ya changamoto zinazojitokeza na jinsi
ya kuzishughulikia. Aina hii ya muda itaruhusu vidato vinne vya elimu ya
sekondari ya kawaida na nane ya
elimu ya sekondari ya juu kupimwa.
Hata hivyo, uhusihaji wa masuala ya
mitihani unaweza ukafanyika iwapo
matokeo ya uhuishaji wa mitaala kwa ujumla utahitaji pia eneo la mitihani
liguswe na kuhuishwa pia. Kwa mantiki hii, viwango vya alama na
ufaulu ni kama inavyooneshwa
kwenye jedwali la 1 hapa chini: Jedwali Na 1 MUUNDO WA ALAMA NA UFAULU ALAMA UWIGO WA ALAMA IDADI YA
ALAMA TAFSIRI
A 75 - 100 26 Ufauli Uliojipambanua
B+ 60 - 74 15 Ufaulu bora sana
B 50- 59 10 Ufaulu mzuri sana
C 40 - 49 10 Ufaulu mzuri D 30 - 39 10 Ufaulu Hafifu
E 20 - 29 10 Ufaulu hafifu sana
F 0 - 19 20 Ufaulu usioridhisha
 
Swali:wale ambao wamemaliza form 4 miaka 5 au 6 iliyopita antaka kufanya ACSEE kama PC hizo CA anazitolea wapi?
 
Swali:wale ambao wamemaliza form 4 miaka 5 au 6 iliyopita antaka kufanya ACSEE kama PC hizo CA anazitolea wapi?

Ili ufanye mitihan ya PC kuna vgezo lazma utmze wanaangalia mpka matokeo yako ya form 2,4,na 6 ndo wanakupa namba ya mtihani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…