Hivi mtu akitolewa mapepo huwa anaelewa na kusikia anayoyasema

Hivi mtu akitolewa mapepo huwa anaelewa na kusikia anayoyasema

simakoku

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
537
Reaction score
586
Nimeshahudhuria mara nyingi maombezi ya watu wanye kutolewa mapepo kwa jina la YESU na nimeshuhudia kabisa watu wakati wanatolewa wakiongea mambo mengi na wengine kujipinda kama nyoka na mambo mengine mengi.

Ila sijawahi kupata bahati ya kuwauliza hiyo experience inakuwaje? Kuna anayejua kama huwa yale wanayoyosema huwa wanayasikua au huwa wanakuja tu kuambiwa baadae kuwa ulisema hivi na hivi, na kuna ambao huwa hata sauti zao zinabadilika kabisa.
 
Ndugu zangu,
Wakati wa misukosuko hiyo ya kupambana na jini,mara nyingi kuna ukosefu wa elimu na utaratibu wa kumtambua kiumbe yule yupo kwa ajili gani mwilini mwa binadamu.Kwa wale majini waliopo kwa minajili ya uharibifu wanayo tabia ya kufunga ufahamu mzima wa binadamu na huzungumza na kufanya mambo mengine bila ya mwenye tatizo lile kujua kinachofanyika.Hii inatokana na jini yule kuwa na hasira ya kuingiliwa kwenye himaya aliyopo kwa wakati ule kwa kazi yake.Hii husababisha mtu kuwa na nguvu sana kiasi cha kuweza kuwasukuma na hata kuwaumiza watu wanaomkamata yule mwenye tatizo.Sasa hapa ndipo kuna tatizo.Utakuta wanaofanya kazi ile iwe ni maombi au "Kukemea" kwao hawawezi kubaini kwamba kiumbe yule yupo kwa shari au amani.Hapa Watendaji wanakosa subira na elimu na kukurupuka kama kinahotaka kufukuzwa ni paka au mbwa.Mwishowe huwa ni purukushani na kuumizwa.Na ikumbukwe kwamba jini yule haonekani na ikiwa ataamua kutulia na kusogea pembeni,mliyofanya kazi ile mtajiona mmeweza bila kujua kwamba jini yule atatoka akiwa na hasira na kwenda ama nyumbani au popote na baadaye kurudi akiwa na ghadhabu maradufu na kumuadhibu binadamu yule kwa namna anavyojua yeye.Hii ni aina ya kwanza ya jini.
Ya pili,kuna jini yupo kwa sababu ni wa asili katika ukoo ule na yupo kwa sababu ya kumsaidia binadamu yule katika maisha yake.Mathalan mtu yule hajijui kuwa anaye kiumbe kama yule.Sasa basi nataka tuelewane hapa.Majini wa aina hii hawafanyi uharibifu ila wanampa wakati mgumu na hata mambo yake kutokwenda vizuri.Na hata ikitokea akaenda kwa watu wenye ujuzi wa kuwatambua viumbe hawa,na inapotokea kiumbe yule kuzungumza mara nyingine binadamu mwenye kiumbe yule husikia na kuelewa kinachofanyika.Utakuta kwamba anampa wakati mgumu mtu yule kwa sababu yapo makosa anayoyafanya kama kutosali,kwenda sehemu za starehe zenye mabo ya ajabu na hata kuwa na mahusiano na wanawake/wanaume zaidi ya mmoja,kutokuwajali wazazi na mengine mengi.Kiujumla kukiuka kulikokithiri kwa mafundisho ya dini.Hapa lazima mtu aonje joto ya jiwe.Na inapotokea mhusika akaenda kwa watu sahihi na siyo kwa makelele na kufukuzana,hapo tatizo litajulikana na jini yule kuzungumza chanzo cha matatizo ya mtu yule ni nini na inatakiwa afanye nini.na ikitokea mkamwelewa jini yule na kutekeleza yaliyosemwa,mambo huwa mazuri na amani kutawala.Lakini ikitokea akapelekwa sehemu za watu kukurupuka na kuanza biashara ya kupigiana kelele,nyimbo na amri za kufukuzana,hapa niwaambie wazi madhara yake kwa aliye na kiumbe yule,waliyo hodari kwa kelele na amri bila kuwa na elimu nalo ni makubwa.inatokea mkaadabishwa kwa namna nyingi.wengine kupoteza mali,hadhi na kazi.hayo ni machache tu katika mengi niliyo nayo
 
Back
Top Bottom