Mzee Gwanda
Member
- Oct 18, 2011
- 26
- 4
Yaani hakuna cha magazeti cjui HABARI LEO, TANZANIA DAIMA, wala ITV. Ni kwamba hii attachment imetoka TAMISEMI kabisa hadi sasa imo kwenye NOTES BOARD. Sasa najiuliza taarifa hii imecombine hata habari za chakula kwa wanafunzi wa bweni kumbe huenda wote ni uongo mtupu hata shule hazina vyakula kweli. Kama mtu anapata ujasiri wa kudanganya wasomi zaidi ya 40,000 kwenye ishu ambayo ni very serious hii nchi inaelekea wapi jamani. Hakuna aliyelazimishwa kutoa taarifa kama hii kwa umma tena. Bora wangetuacha tukaendelea kusubiri kimya kimya kama ilivyokuwa na tetesi zikaendelea za HAKUNA AJIRA kuliko kudanganywa kama watoto wadogo. Athari za uongo huwa kubwa sana make wengine walokuwa PRIVATE tayari wamekimbia wakijua tar.25 wanapata post kumbe SIASA. I hate politics in serious issue, I hate politics and I'll hate it forever.