Ziroseventytwo
JF-Expert Member
- Mar 27, 2011
- 8,581
- 15,618
Sisi ni wafanya biashara ya mazao, tunanunua mazao kwa wakulima kule ulanga,tunalipa ushuru wa mazao wa tsh 2500/= kwa gunia hii ni kwa wilaya ya Ulanga. Tuikifika hapa ifakara, baada ya kukoboa tunalipa tena tsh 3000/= kwa gunia ushuru wa mazao hii ni kwa wilaya ya Kilombero. Ukifanya hesabu, gunia 100 utalipa tsh 250000/=(ulanga huko) ukikoboa gunia 100 unapata kgs 7200 au gunia 72*3000=216000+250000 za ulanga unapata 466000/= na siku za karibuni kuna watu/wahuni wapo pale kibaha mail 1 kwenye mzani, wanatusumbua eti wanataka leseni/kibali cha kusafirisha mazao! Swali, hivi hizi tunazolipa kodi/ushuru tunalipa mara ngapi? Inakuwaje bidhaa 1 ilipiwe kodi/ushuru mara 2? Kwani mpunga si ndio mchele? Tafadhali mtu anayejua elimu ya mlipa kodi anijuze?