Hivi mtu aweza kurithi Ugonjwa wa Kansa?

Dickson Ng'hily

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2010
Posts
451
Reaction score
485
Wakuu naomba msaada hapa, hivi mtu awezarithi ugonjwa wa kansa? Nasema hivi juu babu yangu mzaa mama alifariki kwa ugonjwa wa Kansa ya Jicho...Shangazi yake mama yeye alifariki kwa ugonjwa wa Kansa ya Kizazi...Mama yangu Mzazi alifariki kwa Kansa ya Ini...Mjomba wangu ambaye mama alikuwa anamfuata kwa kuzaliwa aligundulika na uvimbe kichwani na ulipochunguzwa akagundulika kuwa ilikuwa Kansa na hivyo kupelekea kufanywa upasuaji ya kuuondoa, lakini vile vile kipande cha mfupa (fuvu) kwani kilikuwa kimeharibika (Kimeoza)....

Sasa najiuliza, je inawezekana hili tatizo lipo kwenye ukoo hasa upande wa kwao mama au! Naomba msaada wenu Tafadhari...
 
Ndio,

Ziko kansa zinazorithiwa.

Ipo kansa ya jicho inaitwa retinoblastoma ambayo ina form inayorithiwa.

Hata zile kansa ambazo hazijaonekana kurithiwa, lakini zimeonekana zina uhusiano wa kifamilia. Hii inaaminisha kwamba inaweza kuwa inarithiwa ila mfumo wake wa kurithiwa bado haujajulikana.
 
Mkuu ZeMarcopolo Sasa hizo Kansa za kurithiwa hazina Dawa ya kutibika hayo Maradhi?
 
Last edited by a moderator:
angelina jolie amekatwa matiti,kwa sababu ana asilimia zaidi ya 80 ya kupata kansa ya matiti,mama yake mzazi alikufa coz of kansa ya matiti.na wewe kaka jicheki mapema,vimelea vya kansa vinaweza kurithiwa
 
du! Hii hatari kwelikweli,, hivi na ugonjwa wa kisukari nao huwa unrisiwa?
 
du! Hii hatari kwelikweli,, hivi na ugonjwa wa kisukari nao huwa unrisiwa?

Ugonjwa wowote ambao si wa kuambukizwa na unahusiana na DNA/ genes unaweza kurithiwa, kwa sababu genes zinarithiwa.

Kwa hiyo kama umo katika familia ambayo ina genes zinazochangia uzalishaji wa insulin kuwa mdogo kwa mfano, unaweza kupata ugonjwa wa kisukari kama waliokutangulia katika familia.

Ndiyo maana kujua medical history muhimu sana.
 
Ugonjwa wa kansa hutokea pale ambapo oncogenes zinashindwa kudhibitiwa, hivyo zinaanza kusababisha seli kugawanyika na kukua spidi kubwa. Pamoja na visababishi vya kimazingira (environmental factors), kama chakula, sumu, mionzi n.k, pia visababishi vya ndani vinavyoendeshwa na genes (intrinsic genetic factors) huweza kusababisha oncogenes zikawa stimualted na kuanza kwa kansa.

Hii inamaanisha uwezekano wa kurithiwa kwa chance ya kupata kansa upo, japo inaweza pia isitokee...
 
Baadhi ya saratani ambazo zinaweza kurithiwa ni pamoja na saratani ya titi, saratani ya mifuko ya kizazi (ovarian cancers), saratani ya nyumba ya kizazi (endometrial cancers), saratani ya utumbo mkubwa (colorectal cancer), saratani ya jicho (retinoblastoma), saratani ya damu (leukemia), saratani ya ubongo, kongosho nk

Kwa hiyo ukiwa na ndugu hasa first degree relative mwenye mojawapo ya saratani hizo, kuwa makini kwa kufuatilia uchunguzi wa mara kwa mara. Kama una guts za Jolie unaweza kuondolewa kiungo kama kinga dhidi ya kansa.
 
Pamoja na kwamba kansa, hypertension na kisukari zinarithiwa, hiyo ni moja tu kati ya risk factors za kupata magonjwa haya. Kwa sababu una tisk factor moja ya genetical, hakikisha unafanya mazoezi ya kutosha, unakula balanced diet na unakuwa na uzito stahiki. Hapo utapunguza chances za kuugua hayo maradhi.
 

Kuna kila sababu ya kuhakikisha elimu kuhusu ugonjwa wa kansa inatolewa na kuwafikia walengwa, Watanzania wengi hatuna awareness kuhusu cancer.
 
Mkuu ZeMarcopolo Sasa hizo Kansa za kurithiwa hazina Dawa ya kutibika hayo Maradhi?

Mkuu Mzizimkavu,

Kutokana na upana wa ugonjwa wenyewe, haiwezekani kuwa na jibu la moja kwa moja. Kutibika kwa kansa kunategemea na tabia ya kansa, organ ziliyoshambuliwa, wakati ilipogunduliwa (stage), hali ya afya ya mgonjwa etc.
 
Zinarithiwa...na si ugonjwa wa kansa tu..magonjwa haya makubwa mfano kisukari same..na kwetu mimi iko kwenye hypertension amayo kwa jina maarufu ni low Pressure ama BP ya kushuka...Baba yetu alikuwa na BP low,watoto wa tatu wa familia tunayo...na wala sisi si wanene kwamba mafuta
 

>Kwa uzoefu wangu ninajua kuwa Cancer hailithiwi kama ilivyo
bali mazingira ya aliyepatwa na Cancer yanauwezomkubwa wa kumfanya mwanafamilia wa muathirika anaye ishi mazingira sawa nayeye kushikwa na Cancer kiurahisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…