Hivi Mungu ametuumba duniani tuje kufanya kazi na kuwa matajiri au masikini? Na kwanini?

Zee la madawa

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2022
Posts
1,895
Reaction score
4,478
Hivi wakuu Mungu ametuumba sie wanadamu tuje kufanya kazi? Na kuwa matajiri? Na kwanini wengine ni matajiri na wengine ni masikini? Na je kuna watu special wameumba kuwa matajiri na kuna watu special wameumbwa kuwa masikini? Na kwanini iwe hivyo?

Na ili kuishi duniani lazima tufanye kazi ndiyo tule? Mbona wanyama hawafanyi kazi na wanakula?
 
Mambo ya utajir na umasikini mmeyaleta wenyewe, haikuwa plan yake.
 
Hakuna Mungu aliyeumba kitu chochote kile.

Mungu hajawahi kuwepo na hayupo.
 
Ya Mungu namwachia Mungu...ila la Wanyama....

Si kwa wote Ila Wanyama wanaokula kirahisi nao wanaliwa Tajiri (gharama ya kula bure ndio wanalipa hivyo) na kwa wengine., ila so wote....kama Simba Kula Yake ni kazi tosha
 
Mbona wanyama hawafanyi kazi na wanakula?
Wanyama wanahaso pia kutafuta chakula. Hawakai tu hivihivi chakula kijilete chenyewe.

Simba, Chui wanahaso kuwinda ili wale. Wasipowinda no food, Na watakufa.

Swala, tembo na wanyama wote wala majani hupambana kutafuta hayo majani ndio wale.

There is no free lunch.

Hustle lazima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…