The Wisdom
Senior Member
- Oct 20, 2011
- 182
- 56
Msaada plz Drs!!
Wife kaanza bleed 27-29/06
so nisaidieni lini na lini hayo mayai yanatoka???
Kabla ya kujibu swali lako, labda utusaidie nasi kujibu hili swali ndio itakuwa rahisi kukupa jibu stahiki...Je mkeo ana mzunguko wa siku ngapi kwa jumla?
Siku 28!
Okay mkuu,
Kawaida siku ambayo yai hupevuka na kushuka kuelekea mji wa mimba "Ovulation" ni siku ya 14 kabla ya siku ya mwisho ya mzunguko wake.
Mathalani;
mtu mwenye jumla ya siku 28, basi ovulation kwake hutokea siku ya 28 kutoa siku 14 [ 28 - 14 = 14]
mtu mwenye jumla ya siku 29, basi ovulation kwake hutokea siku ya 29 kutoa siku 14 [ 29 - 14 = 15]
mtu mwenye jumla ya siku 30, basi ovulation kwake hutokea siku ya 30 kutoa siku 14 [ 30 - 14 = 16]
nakadhalika na kadhalika....
Sasa wakati mzuri wa kufanya mapenzi kwa wale watafutao mtoto, iwe ni siku tatu kabla ya ovulation, siku ya ovulation yenyewe na siku tatu baada ya ovulation.
Kwa maelezo zaidi fungua huu uzi hapa chini, kuna mdada mmoja tulishawahi kumpa ushauri na mambo yake yakatick...
https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/418487-msaada-tarehe-ya-kupata-mimba.html
nashukuru mkuu nimekupa feedback muhimu mwisho wa siku!!
Labda kwa kukuongezea tu, kwa kuwa mkeo ana mzunguko wa kawaida ambao ni siku 28 basi most likely ataovulate siku ya 14.
Siku huwa zinahesabiwa kuanzia siku ya kwanza ile ambayo mwanamke anapata bleed...
Labda kwa kukuongezea tu, kwa kuwa mkeo ana mzunguko wa kawaida ambao ni siku 28 basi most likely ataovulate siku ya 14.
Siku huwa zinahesabiwa kuanzia siku ya kwanza ile ambayo mwanamke anapata bleed...
umetisha Mkuu hapa nimejifunza kitu, maana mim hiyo siku ya 14 mimi ndo nilikuwa namuomba game wife kumbe mchaka mchaka unatakiwa atleasta 3dyz nyuma!
Thnx!!
Kuwa na uhakika zaidi ni vyema kuanza mapema na kuendelea siku chache baada ya ovulation...
Nimeandika hivyo kwa kuwa wakati mwingine hutokea kuwa ovulation hubadilika, na husababishwa na vitu kadhaa kama mabadiliko ya mazingira na hali ya hewa, mabadiliko ya utowaji wa hormones mwilini n.k