Hivi mwanamuziki Senzo yu hai au alishafariki?

Senzo yu ngali bado hai isipokua kuna maradhi yalimpata mpaka kupelekea kusitisha shughuli zake za mziki.

Nadhani mwaka jana kama si mwaka juzi alifanyiwa mahojiano na mwandishi mmoja wa habari huko South Africa nami nikafanikiwa kuyatazama.

Hebu ingia YouTube andika neno Senzo ili na wewe upate kuona na kusikiliza kile alichoongea.
 
Senzo amefariki muda mrefu na aliuwawa kwa kupigwa risasi na rafiki yake kipenzi aliyekuwa anampa drugs anaitwa LONGWE drugs zilikuwa zinamsaidia kupafomu muda mrefu.

Ugomvi ulianzia kwa mmoja wa rafiki yao anaitwa kelly dhidi ya Longwe kisa tu mwanamke sasa ikabidi aingilie Senzo na wakati huo alikuwepo mwanamke ambaye ni mama yake na kelly khumalo.

Longwe alimpiga risasi Senzo na baada ya kumpiga aliwatishia kelly na mama yake kuwa wakisema atawauwa nao.
Maneno ya mwisho aliyoyatamka senzo ulimwenguni ni "yini le oyenzayo mfethu" (What are you doing my brother)
 
Hapana ameuwawa muda mrefu ni miaka mitano sasa
 
Mkuu huyu Senzo unaemuongelea hapa sio Artist jamaa aliyeuliza bali ni goolkeeper (Footballer) wa Bafanabafana,Senzo anayeongelewa ni yule mpiga vyombo wa Luck Dube na baadaye alijitenga na kuanzisha band yake mwenyewe,baadhi ya nyimbo zake maarufu ni WHO IS GONNA CARE FOR YOU & I, I'LL BE THERE,JAH GUIDE.
 
To add up,hungry lions,holly place ,guilty,jah is love,,me and my guiter,rasta wake up,thank you,thanks and praise,the way life goes,,new love etc
 
Huyo Senzo unayemuongelea hajawagi kupiga "vyombo" kwa Dube!

Jamani Meneja wa Dube yupo wanae, hata historia ya wanamziki waliowahi kufanya kazi na Dube ipo mitandaoni! Senzo hakuwahi kuwa na Dube!

Mwisho hajafaaa, mbona mnapenda story za vijiweni!!

angalia performance live ya huyo mnaedai alikufa!

Kafanya mwaka huu
 
Aisee, hata mimi nilijua ameshafariki.. Ila leo ndio nimejua kuwa bado huyu jamaa yupo hai, dah. Ingia fb kuna page inaitwa Senzo Mthetwa kuna taarifa za kukanusha kifo chake pia wameweka namba za simu za sister ake ili kuprove kuwa yu hai, mcheki, 0838008189. Taarifa mbaya husambazwa haraka kuliko nzuri. Ama kweli bora walimaharage kuliko walimwengu.
 
Huyo wakutengenezwa,,Senzo wa Jah guide,alisha rest in peace kitambo,,,,Ila si kimwili bali kimuziki..Du duniani kuna mambo.
 
Senzo nayemuongelea ni mwanamuziki wa reggae na ni marehemu hivi sasa
 
Senzo yuko hai na anawalaani sana sana mnaodai amekufa! Mfuatilie YouTube, Facebook na mwezi July mwaka kuu ana perform live huko south Africa.

Acheni kundekeza minong'ono! Senzo yuko hai hakuuliwa wala hakuua!
Senzo hayuko duniani tena toka 2015.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…