Hivi "mwanazuoni"ni mtu wa aina gani

Hivi "mwanazuoni"ni mtu wa aina gani

wa stendi

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2016
Posts
25,190
Reaction score
27,434
Hua nasikia kwenye matangazo mbalimbali kama matamasha au maombi fulani au semina wakitangaza baadhi ya viongozi au waaalim fulani wa huchi kipindi wakati huohuo watasema pia kuna mwanazuoni au wanazuoni kutoka sehem au taifa lingine kuwa ataudhuria kwenye hilo somo je!huyu "mwanazuoni"ni mtu wa aina gani??au anashughulika na nini hadi anaitwa mwanazuoni.
 
Japo sina hakika sana...nadhani ni wale wasomi waliobobea katika masuala mbalimbali na wenye elimu kubwa
 
Intellectual...mtu mwenye uwezo mkubwa kiakili.
 
Mwaanazuoni ni mtu aliyebobea katika tasnia fulani. Ni neno lililoaza kutumika zama na zama. Kwa leo wanazuoni unaweza kusema ndio maprofesa.
 
Ni kama mimi hapa.


Watanzania daini katiba mpya vinginevyo mtapata tabu sana.
 
.
mwanazuoni ni mtu anayetumia elimu yake kukusanya, kuchambua na kutolea mapendekezo ya kitaalamu masuala yanayojitokeza ktk sehemu fulani ya jamii. Msomi ni mtu aliyekwenda shule kwa kiwango stahiki lakini yupo disconnected na jamii yake- Issa Shivji kigoda cha sita kama sikosei
 
Mwanazuoni/ Mwanachuoni/aalimu pia Ulama, kwa mujibu wa KAMUSI YA KISWAHILI SANIFU(Toleo la Pili,2004) Uk.219.

Mtu ambaye ana utaalamu wa kiwango cha juu wa somo au maarifa fulani.
 
Back
Top Bottom