Hivi mwenge bado unamulika wezi ,wala rushwa na mafisadi kama tulivyoaminishwa zamani?

kimyamana1981

Member
Joined
Apr 14, 2025
Posts
31
Reaction score
18
Habarini wakuu,

Najiuliza kuwa hivi mwenge bado unamulika wezi,wahaini,wala rushwa na mafisadi kama tulivyoaminishwa zamani. Bado upepo haujakata masikioni juu ya tuhuma alizotoa CAG za ubadhilifu, hao wabadhilifu mwenge haukuwaona?

Nimeshuhudia migambo na askari wanalazimisha watu wafunge biashara zao waende kwenye mwenge hii ni haki?

Hivi mpaka sasa mwenge una faida gani katika uchumi wa mtanzania mmoja mmoja?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…