Msimu huu Yanga Wana pointi moja wameitoa wapi mkuu?
We jamaa unasoma kuelewa au unasoma kubishana? Maana nimeweka wazi kila kitu lakini bado kichwa chako kigumu kuelewa. Nimekwambia 5 year ranking inafanyika kila msimu mpya unapofikia. 5 year ranking kuelekea msimu wa 2021/2022 imechukua point ya misimu mitano nyuma ambayo
Ni msimu wa
1)2020/2021
2)2019/2020
3)2018/2019
4)2017/2018
5)2016/2017
Ndani ya hiyo misimu mitano Yanga walipata point 0.5 hivyo hizi point zinazidishwa na coefficient ya mwaka yaani
Msimu husika inakuwa na coefficient5
Msimu wa pili kutoka juu una coefficient 4
Wa tatu kutoka juu una coefficient 3
Msimu wa nne toka chini una coefficient 2
Msimu wa mwisho kabisa unakuwa coefficient 1
Hivyo kwa 5 year ranking ya msimu wa 2020/2021 Yanga wana point 0.5 zidisha kwa mbili inakuwa point 1 .
Baada ya timu kuingia hatua ya makundi katika msimu huu wa 2021/2022
CAF wanafanya tena 5 year ranking ambayo itatumika katika mashindano ya msimu mpya wa 2022/2023. Point zinachukuliwa kwa walioishia makundi mpaka kwa aliyechukua kombe msimu wa 2021/2022. Hapa CAF wanachukua tena matokeo ndani ya misimu mitano kwanzia msimu wa 2021/2022 mpaka msimu wa 2017/2018. Zile point 0.5 za yanga hazitozidishwa kwa coefficient 2 bali zitazidishwa kwa coefficient 1 na kuwa ni 0.5 .