Kikwete kipindi chake shule za kata ndio kwanza zilikuwa zinajengwa. Uhaba wa walimu ulikuwa mkubwa kupindukia, kabla hakuna graduates wa BaED tiyari wanapigiwa mahesabu wakazibe viraka wapi.
Sensa ya mwaka 2012 Tanzania ilikuwa na watu milioni 45. Sensa ya 2022 Tanzania watu milioni 60. Bajeti ya kujenga shule na hospitali, afya, chanjo ni kubwa zaidi. Vipaumbele vimehama kutoka kuajiri kwenye upungufu na sasa vipaumbele rasmi vya awamu ya sita bado maana mzigo ulioachwa na awamu ya tano ni mkubwa na unatugharimu sana kwa bajeti na fedha za kigeni. Awamu ya tano ilikazania ujenzi wa miundombinu, flyovers, SGR, bwawa, madaraja, mji mkuu, n.k.