Hivi na hili SUMATRA inalijua? Tuisaidie, pengine meno yataota

Hivi na hili SUMATRA inalijua? Tuisaidie, pengine meno yataota

Boeing

Senior Member
Joined
Apr 16, 2017
Posts
151
Reaction score
422
1.Mabasi yanajaza kupita uwezo,ushahidi Upo, ni juzi tu nimesafiri kuelekea mbeya kwa basi mojawapo,wanaweka ndoo kibao. Traffic wanapewa chao mambo yanaenda kama kawaida
2. Kuna gari aina ya noa, zimebadilishwa na kuwa za abiria. Kiuhalisia ile gari ina capacity ya watu 8 ila inabeba 10. Traffic wanakagua ticket na magendo wanaona kuzidisha abiria ni sawa.
3. Nauli siku hizi wenye magari ndo wanapanga na sio Sumatra kama awali. Mfano barabara kama haikuwa na lami then ikawekwa lami tunategemea nauli zipungue ila unakuta inabaki palepale au inapanda zaidi. Yapo mengi sana hadi yanakera

My take; serikali inapaswa kuiangalia Sumatra upya. Iwe strict kwani uzembe wa chombo hiki unagharim nguvukazi ya taiga.
 
Sikuiti Mnoko Mkuu lakini haya uliyoyasema yapo kabisa!Natamani wahusike wapitie hapa ili waboreshe
 
Umesahahu abiria kukaa siti ya dereva na kwenye BUTI. Haya hufanyika kwa wenye NOAH na COROLLA
 
Tunalishwa chakula wanapotaka wao na kwa bei wanazozijua wao.

Sumatra hawana msaada kwa abiria zaidi ya kuwa kiungo kati ya wamiliki na Serikali na ni kwa vile wametega hela ndio maan matatizo kwao mtaji.

Faini ya gari lililojaza abiria inawezwa kulipwa na abiria watano waliozidishwa kati ya ishirini, kwa hyo kwa wenye mabasi hakuna hasara.

Kama wanaweza iwe gari likizidisha safari itaendelea kesho, uone kama abiria watakubali mtu asye na siti apande.
 
Sumatra hawana msaada kwa abiria zaidi ya kuwa kiungo kati ya wamiliki na Serikali na ni kwa vile wametega hela ndio maan matatizo kwao mtaji

Sumatra ni chombo cha kupiga dili tu hamna chochote
 
Nawaalika SUMATRA waje kituo cha mwendokasi Kimara kuanzia SAA moja asbh hadi SAA NNE waone vile watu wanazimia kwa kukosa hewa kwenye hayo mabus....maana naamini yangekuwa ya binafisi yashafungiwa kitambo
 
Kuna route ya Mwanza-Kampala, owner wa route ni FRIENDS Express(Sanlait Uganda Ltd), mkifika Geita (sometimes) unashangaa wanaingia abiria wengi sana wakiwa na ndoo zao za lita 10 hivi wakiingia on board wanazipanga ndoo zao kwenye Aisle wanatulia kwa raha zao, mara ya kwanza nilidhani wanafuata maji. Kote mnakopita trafiki husimamisha chombo na huishia mlangoni tu. Mungu asiruhusu ya kivuko kutokea huku nako...
 
1.Mabasi yanajaza kupita uwezo,ushahidi Upo, ni juzi tu nimesafiri kuelekea mbeya kwa basi mojawapo,wanaweka ndoo kibao. Traffic wanapewa chao mambo yanaenda kama kawaida
2. Kuna gari aina ya noa, zimebadilishwa na kuwa za abiria. Kiuhalisia ile gari ina capacity ya watu 8 ila inabeba 10. Traffic wanakagua ticket na magendo wanaona kuzidisha abiria ni sawa.
3. Nauli siku hizi wenye magari ndo wanapanga na sio Sumatra kama awali. Mfano barabara kama haikuwa na lami then ikawekwa lami tunategemea nauli zipungue ila unakuta inabaki palepale au inapanda zaidi. Yapo mengi sana hadi yanakera

My take; serikali inapaswa kuiangalia Sumatra upya. Iwe strict kwani uzembe wa chombo hiki unagharim nguvukazi ya taiga.
Tatizo muda huu ni highseason watu wanasafiri sana na magari ni machache, mi naona abiria ndo wenye makosa wanataka kusafiri kwa kulazimisha ilimradi wafike
 
Kwanini upande kama gari limejaa, mimi ninauhakika hata wewe ungekuwa dereva ungezidisha ili upate posho, kumbuka hao madereva hawana mshahara wanaishi kwa posho
Tunalishwa chakula wanapotaka wao na kwa bei wanazozijua wao.

Sumatra hawana msaada kwa abiria zaidi ya kuwa kiungo kati ya wamiliki na Serikali na ni kwa vile wametega hela ndio maan matatizo kwao mtaji.

Faini ya gari lililojaza abiria inawezwa kulipwa na abiria watano waliozidishwa kati ya ishirini, kwa hyo kwa wenye mabasi hakuna hasara.

Kama wanaweza iwe gari likizidisha safari itaendelea kesho, uone kama abiria watakubali mtu asye na siti apande.
 
naona siku mbili hizi mada za kuikumbusha serikali zimeshamiri kwelikweli kisa ile ajali ya mv nyerere. acheni unafiki mpaka muone tukio ndio muanze kutoa ushauri. ngoja tumalize mazishi kwanza labda tutawasikiliza.
 
SUMATRA NI JANGA KWA TAIFA HILI! Hawana Utashi, Weledi hata Uwezo wa kusimamia idadi ya abiria katika vyombo vya usafiri nchi kavu na majini! Nadhani wakati umefika kwa JPM kupangua safu nzima ya Taasisi hii inayo fedhehesha na kuliabisha taifa kwa utendaji wake mbovu!
 
Back
Top Bottom