Bright
Member
- Apr 9, 2010
- 67
- 0
Uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 sikupiga kura kwani uchaguzi ulikuwa wa wazi. CUF na DP waliongelea hili mara moja tu na kukaa kimya pengine baada ya kupewa nakala ya daftari la wapiga kura. Katiba yetu inasema kura ni ya siri lakini upigaji kura unakuwa wa wazi. Je huku sio kuvunja au kuisigina kabisa katiba ambayo wengi wa viongozi wa juu akiwemo M/kiti wa tume ya uchaguzi waliapa kuilinda huku wakiomba Mungu awasaidie? Mimi nafikiri kimoyo moyo wanaomba Shetani awaongoze kwa kutokana na wanayotenda! Mtikila mbona hujapeleka hili mahakama kuu?
Muda mfupi kabla ya uchaguzi, nilikutana na mwandishi wa gazeti moja na kumwambia kwa nini hawajaliandikia hili wakati Mtikila na Hamad walishaongelea suala hili; alijibu na kuwa muwazi kuwa labda wananchi wapitishe 'petitions' lakini vinginevyo alikiri kuwa wataingia matatani!