Hivi ndio ndoa zilivyo?

Kubembelezwa pakiwa pa upande mmoja tu kila mara panaboa bana.
 

Tuna kama miaka 3 nyamayao ila ndo katabia chake kila tunapopishana maneno bila mi kushuka akieleweki.
 
Yani mpaka mnakula sahani moja??Aisee!Nwy mwambie kama baba umeamua kwamba aachane na mkopo baada ya mwezi au miwili mtanunua hivyo vitu!Then usimbembeleze kwa zaidi ya wiki mbili uone kama ataendelea kununa.Kama ataendelea mwisho wa siku bembeleza ukijua siku ukimkosea kikwelikweli utashaa!
 
mbembeleze, acha kuwa ngangari!!wanawake ndio walivyo na ndicho anachotaka. tena usiache fanya haraka. utapoteza ndoa ukichelewachelewa
 
Uwe makini kdg,huenda kuna 'jamaa' kamwahidi kumpa,so anatafuta baraka zako kiaina 'while hiding her head in the sand' usije shangaa mabadiliko ya ghafla.Mkubalie/mtege auchukue muuweke bank mtapata hiyo interest.Check hiyo salary slip km ina deductions,km vp umeliwa.
 
Mtafutie msaidizi haraka vinginevyo atakuendesha sana
 
Ni vizuri kama ushajua kuwa akinuna anahitaji kubembelezwa ili awe sawa.
Mbembeleze.
Kwani kumbembeleza inakugarimu nin?
Katika mapenzi wote mkitaka kujifanya mpo juu kama kikombe cha babu hamtafika popote.

Sawa lakini huoni basi akizoea hivyo itakuja kuwa ndo tabia kwamba ye hatak kushauriwa ukipishana nae tu ye atakuwa ananuna sasa tutaenda hivyo mpaka lini sasa au mwisho wake ni nini?
 

...Una bahati sana wife wako kakushirikisha kwenye mipango yake ya mkopo.
Wenzako wanakopa na kujiendeleza kivyao. Shukuru mungu kwa hilo kwanza.

Pili, shukuru mungu mkeo ana mipango ya kuboresha maisha yenu kwa uwezo mlio nao sasa.
Hiyo kauli ya Ipo siku, hata siku moja haitakuja timia bana. Ipo siku ni kauli ya waliokata tamaa.
You only have "today" to live! Ya kesho huyajui, wasiwasi wa nini? Ya kesho yatajitatua yenyewe.

Chanzo cha mkeo kununa inawezekana ni hiyo tabia yako. Kila anapokushirikisha kwenye jambo,
wewe unakuwa ni muamuzi wa mwisho. Tabia mbaya sana, Acha nae awe na maamuzi yake,
Ndio Uhuru wa ndoa huo. Taratibu isijefikia mke akajiona hana kauli ndani ya nyumba.

Kubali achukue huo mkopo mboreshe maisha yenu ya leo.
 
Tuna kama miaka 3 nyamayao ila ndo katabia chake kila tunapopishana maneno bila mi kushuka akieleweki.

kwa ukweli inaboa sana, ningekuwa ni mie wewe ningemchunia mpaka atakapoona imekuwaje then aanze kujiongelesha, hapo unampa fundisho kwamba hatuendi/hatutaweza kuendelea hivi akiwa anajitambua atabadilika, kinachomfanya mgumu kubadilika ni vile kila wakati unavyombembeleza hata kama ishu ni yeye kaifanya, kama hapa mie cjaona ishu kabisa kabisa, sasa mtaishije ndani bila kushauriana?...na nani kamwambia watu wanakopaga pesa kununua furniture za ndani, pesa inakopwa kwa ishu za muhimu jamani, kumalizia kakibanda/cjui mmekwama fees...sasa ununue sofa zina ulazima gani kwa wakati huo?
 
Naamini siwezi kumchunga mtu mzima so huwa si hofu kabisa eti labda wife anakidume au lah ila naamini za mwizi 40.
 
mbembeleze, acha kuwa ngangari!!wanawake ndio walivyo na ndicho anachotaka. tena usiache fanya haraka. utapoteza ndoa ukichelewachelewa

tunapenda kubembelezwa but sio kwa ishu kama hizi.
 
Naamini siwezi kumchunga mtu mzima so huwa si hofu kabisa eti labda wife anakidume au lah ila naamini za mwizi 40.
Inabidi uwe makini maana huwezi juwa..
 
Sawa lakini huoni basi akizoea hivyo itakuja kuwa ndo tabia kwamba ye hatak kushauriwa ukipishana nae tu ye atakuwa ananuna sasa tutaenda hivyo mpaka lini sasa au mwisho wake ni nini?

ukishasawazisha ya sasahv tafuta muda mzungumzie juu ya hilo suala lake la kununa nuna.
 
kaka akili zako kichwani hapa utaambiwa mambo kibao ni wewe kuchuja, mambo cjui ya kumtafutia msaidizi cjui nn na nn sio kutatua tatizo bali kuongezea tatizo juu ya tatizo.
 
Reactions: Mbu

...paranoia na suspicious minds hizi mnazipandikiza vichwani halafu zinamea na kuzalisha dhahma kwenye maisha ya ndoa. Taratibuni msijegeuka wanaume ambao hamtaki mke akuzidi kielimu, mali wala busara.
Kununa ni non-verbal communications.

Kama unampenda Mkeo/Mumeo, utajiuliza kwanini kanuna na wewe umechangia lipi.
Kesi hii ipo wazi kabisa, Mke ni Optimistic wakati mume ni Pessimistic. Clash of characters.

Manuu, ni Lazima uuchukie 'umaskini' kwanza ndipo mtapoweza kuishi kwa raha na amani.
Msikilize na mpe fursa mkeo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…