Hivi ndio ndoa zilivyo?

Kama unaweza kununua hivyo vitu ulikuwa unasubili nini? Usikute nyie ndo wale wanaume ndani kuna vigoda, maana kama mgekuwa na vitu kwa nini mkeo anunue vingine. Nina kaka yangu ana kazi nzuri na pesa za kumtosha, mkewe ana kazi ya kawaida (graduate) ila ana piga madili sana. Sasa wife hawezi kununua asset yoyote kaka hataki. Matokeo yake wifi anajijengea majumba tu kivyake vyake afanyeje na ela anayo. Huyo kaka sisi tunamjua ana inferiority na kujiona yeye mwanaume kwa hiyo mkewe akichangia maendeleo labda atamtawala.

 
Kuna wanaume bwana yaani akikuoa basi huna maamuzi tena. Mimi hubby alianza katabia ka kunifanya ni loose all my confidence. Yaani nilikuwa fashionista fulani hivi lakini toka kanioa anataka hata nikienda kununua nguo yeye ndo achague. Na mimi kwa mapenzi nilonayo nikawa siwezi fanya kitu mpaka aaprove. Sasa hivi nimeshtuka kwani nimekuwa kama zuzu I can't make my owm decision wakati yeye anachoamua si mpaka mimi ni approve. Jamani kwenye maisha ya ndoa tusipende kubadilishana hivi let your wife, husband "be" him/heself ndo mta enjoy life. Otherwise ndo unakuta mtu anjuuuta kuolewa/ kuoa.
 

sa kama umeshamruhusu kuchukua huo mkopo, ananuna kitu gani??
 
Mh,huyo kuna jamaa anamlisha huko na kahitaji hela ndo mbinu ya kuzipata hiyo!
Ukimruhusu tu utasikia anakwambia kaibiwa
Inawezekana pia kaongwa (kachuna buzi) sasa anashindwa jinsi ya kuzileta home
 
Mkuu wala hujakosea ndoa ndivyo ilivyo hapo hakuna maswali...kama unataka ushauri chukua hii naomba ni mnukuu husninyo "Mbembeleze.
Kwani kumbembeleza inakugarimu nin?
Katika mapenzi wote mkitaka kujifanya mpo juu kama kikombe cha babu hamtafika popote.

Chukua hiyo na kila kitu kitakuwa shwari
 
Wanaume msiwe wajinga kiasi hicho? Ebu nambie huyo mkeo unambembeleza nini? Kwa kipi kikufanye wewe uwe mtumwa wake? Ushauri mzuri umempa hataki mwache achukue mkopo wake aone kero ya kurudisha siku amebauns basi ndiyo unamkumbusha ile habari ya kwa nini hukupenda achukue mkopo wakati mnaweza kujiunga unga ndani ya mwezi mmoja mkapata hiyo mihela.

Wanawake wengine bwana wakipata wanaume wazuri wenye hekima wanacheza. wengine hawapewi ushauri wala kubembelezwa na bado wananyenyekea!

Kaka eeeh! chapa mwendo akiamua kuongea ataongea asipotaka wewe yanakuhusu nini bwana, hakikisha amepika, anafua, anaangalia watoto, na kila kitu cha ndani kinaenda sawa ndiyo anune vizuri sasa. kama hafanyi take a step.
 

Nimecheka sina mbavu!!! Jamani huyu mdada anachezea shilingi chooni..... ana bahati mumewake anamsikiliza na kumpa ushauri du kweli penye miti hapana wajenzi........ Kaka nakushauri ili aache hiyo tabia mbovu usimbembeleze kabisa!!! na shikilia msimamo wa kumkatalia ili mwisho wa siku ajue kwamba kununa au kutonuna kwake havibadilishi msimamo wako wewe kama kichwa cha nyumba
 
Jamani kwani bibie amefanya kosa gani, kama ni makochi kununua si katika kuboresha muonekano wa nyumba yenu?
Mpende mkeo kwa kum support hilo jema analofanya, acha kumnunia.
Wewe subiri mpo mmepumzika wawili, faragha, mbembeleze mkeo
Ndoa inajengwa kwa mmoja kuwa mnyonge, kujishusha inapobidi
 
Nimejaribu kumchunia hadi sasa nahisi kama vile naanza kumchukia
Bado unachuna baba eeh?weeh endelea tu kuchuna kwa ushauri wetu,afu ujue mwenzio ataanza kutafuta wa kucheka nao.Utakapoanza kulazwa njaa urudi hapa tukupe ushauri mpya!weeh mbona mkeo anajua unapenda makande na anakupikia,ukimbembeleza utapata hasara gani?karaha jipe mwenyewe,for whatever reason.
 
Kha mie mtu anayenuna simpendi sana kwa sababu anakuwa na kinyongo mno na huwezi kujua anawaza nini.

Jaribu kumchunia na wewe kutoombwa acha kununa uone kama ataweza kununa mwezi mzima anakutega tu huyo na anajua utambembeleza.

Pole mwaya

Aaaaa. Dena mwenzio dume huyooo
leo mhandisi wangu umegonga na wewe
 
Ni kweli mbembeleze na kila wakati mkumbushe majukumu yake, hawezi kuwa ananuna kila wakati kwa kuwa anakufanya wewe kama mtumwa wake. Love is two ways traffic, zaidi ya hapo basi unakuwa mtumwa, kila siku unafikiria jinsi ya kumfurahisha yeye, bila ya yeye kujali jinsi ya kukufurahisha wewe. Kwa wale mnaopenda kubembelezwa na kubabaikiwa kama MARICHUY, be careful, huwezi jua, MIGUEL anaweza akachoka, na hapo itakuwa too late. Matokeo yake ni kutafuta mapenzi ya HAWARA nje ya ndoa yako, kwa kuwa mahawara wanajua sana kubembeleza (ingawa hawajui kubembeleza wake/waume zao ama sivyo wasingetoka nje ya ndoa zao). LOVE IS GIVE AND TAKE, OTHERWISE, ITS TURNS OUT TO BE SLAVERY.
 
Ndoa haziko hivyo... ni wana ndoa wenyewe wanaofanya ziwe hivyo!
 
Mkeo anapenda kubembelezwa, mbembeleze! Ila tengeneza mazingira ya kuwa baba halisi wa nyumba, mambo ya kununiana ndani ya house sio dili, Huo anaofanya mkeo ni ubabe!
 

Hapo kwenye bluu, Well said king'asti
 
ndugu usimwendekeze hata kidogo kwani umeshampa alternative kakataa basi ana yake huyo.kwani hivo vitu vina haraka ghani hadi akatae kusubiri ushauri wako??? ukimkubalia achukue mkopo kesho atakuambia lingine ukikataa ananuna tena,si unajua silent is the answer for the stupid?? kwa vile ww huna kosa endelea na msimamo wako atakuheshimu na atajiona mjinga kwa kutokukusikiza...ndoa ni kuelewana sasa kwann yy angangane tu?????
 
aaaaaaah kununa ndio hulka yao hawa mi nshazoea, manake siku kama ya leo shurti ukae na wapwa mgonge mvinyo sasa unaporudi tegemea kununiwa
 
AD afanye nini? ampikie,yaani mke wangu akinuna nimpikie na kufuli nimfulie? gggrrrrrrrrrrrr natamani nikumeze AD!
 
Huyo mkeo anatatizo inaonesha hapendi kupingwa katika mawazo yake kama ulivo sema mkitofautiana tatizo. Kifupi mweleze tu tabia ya anachotaka yeye ndo kifwatwe hata kama hakina manufaa kibaya. Pia yawezekana mkeo ni limbukeni na ela kisha hazina liba anataka akope tu hata kama hana shida ya msingi. Last wisemen sometimes change his mind but foolish never. Mkeo atakuwa anaangukia hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…