Hivi ndivyo gari huwa zinawaka moto

JituMirabaMinne

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2020
Posts
3,381
Reaction score
9,744
Hii ni Audi A3 2.0 TSI Hatchback ya mwaka 2010. Nimeifanyia Diagnosis kama kawaida ina error codes kibao (Zaidi ya Faults 50).

Sasa katika kwenda kutest waya za mojawapo ya sensor ambayo ilionesha ina shoti, Pembeni kidogo ya battery si nikakuta moshi unafuka. Halafu lile eneo la fusi box nikakuta ni la moto balaa.

Anyway nmefungua mfuniko wa fuse box ndio nakutana na kitu hiki hapa chini.

Your browser is not able to display this video.


Ikabidi nizime gari then nifanye mpango wa kuchomoa hivyo vibati vilivyobakia hapo maana lile plastic lote la fuse limeshayeyuka na limeanza na kuyeyusha sehemu ya fuse box.

Nikakutana na kitu hiki [emoji1484][emoji1484][emoji1484][emoji1484][emoji1484]



Aiseee ukitazama vizuri hicho kibati kina nyaya nyaya ambazo zimewekwa na mafundi.

Kama kawaida mtu aliona fuse imeungua akaamua kunjunga na mayokeo yake waya umepata current kubwa then moto umeanza. Gari nyingi fuse zake zimezungushwa waya kama ilivyofanywa hii.

Other pictures










Kama kawaida naendelea kusisitiza. Gari za ulaya siyo za kununua kama unanunua nyanya.

Rejea [emoji1484][emoji1484][emoji1484]

Thread 'Gari za Ulaya/Marekani hazitaki ubabaishaji kabisa' Gari za Ulaya/Marekani hazitaki ubabaishaji kabisa

Sasa hebu angalia faults za hii ya leo.









Pia hizi siyo gari za kuendesha tu ilimradi unaona inatembea. Check up inamatter sana. Otherwise siku ukija kupima ndio utatajiwa matatizo mpaka kichwa kikuume.



Kama una tatizo na gari yako au unahitaji Diagnosis nicheck.

Iwe gari yoyote ndogo ya Ulaya, Asia au Marekani tunapima na kusolve.

Nipo Dar.

0621 221 606.
 
Diagnosis mna charge kiasi gani ??
 
Lengo la kuweka nyaya laini au ndogo ili itumike kama fuse ni kwa ajili ya kumtoa mtu porini tu ila kama mtu yuko town huu ujinga hautakiwi.

Na wengi wetu kukadiria ni shida, unakuta mtu anaweka nyaya za kutosha ili fuse isikate tena...

Halafu kuna kitu huwa najiuliza sana, mbona mafundi wengi huwa wanabadili fuse tu pasipo kutafuta sababu ambazo zimepelekea fuse hiyo kukata, wao wana replace tu. Hii imeekaje kaka mkubwa?
 
Ga Gari za Ulaya kwa hela za Mkopo wa NMB Lazima uwe mwehu
 

Kukadiria waya ni kitu kigumu. Ndio maana haishauriwi.

Mtu ajitahidi tu atembee na fuse za akiba...

Fuse kuungua ni kitu cha kawaida ikiungua weka nyingine... Shida ni pale kila fuse unayoweka inawaka moto, Hapo ndio lazima utafute sababu ni nini na mara nyingi sababu huwa shoti...

Kama fuse inaungua mara kwa mara ukiweka waya kama hivyo lazima usababishe moto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…