Hivi ndivyo ilivyo. . . . .!

Eiyer

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2011
Posts
28,259
Reaction score
20,891
Tangu tukiwa na umri wa siku moja,tunataka kukubaliwa,kupokelewa na kulindwa.Haya ni kama mambo ya kimaumbile kwa mwanadamu.Unapogundua kuwa watu wote hawakupendi utababaika na kuchanganyikiwa na maisha kwako yanaweza kupoteza maana.Wengi tunafanya tunayofanya au kuacha kufanya katika kutafuta kupendwa.Kwahiyo kila mmoja wetu ana kiu kubwa ya kupendwa.(hapa nazungumzia kupenda kuliko zaidi ya ule wa ngono)Hapa ndipo linapochipuka tatizo kubwa linalofanya wengi kushindwa kujua kupenda ni nini.Hushindwa kwa sababu hakuna anaejali kupenda,karibu wote tunajali kupendwa,siyo kupenda.Kama nguvu zetu zote tumeziweka kwenye kupendwa,kupenda kunakuwa na nafasi gani kwetu?Ndiyo maana wengi hatujui kupenda,tunangoja kupendwa.Mume anasubiri mkewe ampende,mke nae anasubiri mume ampende!Ni kitu gani kinatokea?Kulalamika kusikoisha.Tumewekeza kwenye kupendwa ambako hakutuhusu.Jambo linalokuhusu ni kupenda,kwani wewe ndo unaamua upende ama la.Kupendwa ni jambo unalofanyiwa,halikuhusu.Yanini uhangaike na jambo lisilokuhusu?Unaposubiri na mbaya zaidi kudai kupendwa,unapoteza muda wako bure kwani unaemtaka akupende nae anataka jambo hilo kwako.Ni jambo ambalo huwezi kulipanga wala kulidhibiti kwa sababu linamhusu mtu mwingine.Inawezekana vp umlazimishe mtu mwingine akupende?Haiwezekani.Lakini tunafanya jambo lisilowezekana.Lakini unaweza kupend kwani ni jambo linalotoka kwako,fanya hivyo maisha yako yote.Mtu akikuambia hakupendi huna haja ya kupandwa presha,au kumnunia na kuwmuwekea bifu,halikuhusu hilo wewe toa upendo tu,hili ndo linalokuhusu!
 
love conquers all na ndio maana maji hupasua miamba.
 
Nimependa kila neno katika uzi wako.
Okay,kuanzia sasa mimi ni kugawa mapendo tu,ni kupenda tu.

Nilichojifunza hapa ni,

UKIPENDA WENZIO NA WENZIO WATAKUPENDA.
 
qeenkami,kanuni ya maumbile inasema unachotoa ndicho unachopata.So ukitoa upendo unapata upendo!
 
Sikupi like, kwasababu nimekupa sana lakini wewe hutoi!

Ila uzi mzuri, jamani mimi napenda sana lkn nmmh!
Ni vigumu kujua kuwa unapendwa au unatamaniwa.
Na shida kuu ya wanaume hamjui kuonesha mapenzi kwa wenzenu, unaassume tu kwa vile niko naye anapaswa kujua anapendwa ndio maana niko naye.
 
ubarikiwe Eiyer, me hupenda kwa kiwango kikubwa!
 
Last edited by a moderator:
Ni kwel uyasemayo LAKINI nitatoaje nischokuwa nacho?
 

Kweli Kaunga nami pia nilikuwa nimempa LIKE lakini imebiedi ni UNLIKE, uzi wake umeeleza vizuri kuhusu kupenda lakini yeye binafsi hajui kupenda ie ku LIKE
 
Kaunga,haya bana we nibanie tu . . .Tupo wanaume wengi sana tunaoweza kuonesha upendo kwa kiwango kikubwa.Pole inaonekana umekutana na wanaume vimeo!. . . . . Nigongee LIKE bana!
 
Je, pendo lako lisipopokelewa na umpendaye unafikiri kupenda kwako kutakuwa na maana sana?
 
Kaunga,haya bana we nibanie tu . . .Tupo wanaume wengi sana tunaoweza kuonesha upendo kwa kiwango kikubwa.Pole inaonekana umekutana na wanaume vimeo!. . . . . Nigongee LIKE bana!

LIKE hiyo chukua
 
Kweli Kaunga nami pia nilikuwa nimempa LIKE lakini imebiedi ni UNLIKE, uzi wake umeeleza vizuri kuhusu kupenda lakini yeye binafsi hajui kupenda ie ku LIKE

Kaunga,unaona unayonisabishia?Sijui utanibebea mbeleko gani. . .
 
Je, pendo lako lisipopokelewa na umpendaye unafikiri kupenda kwako kutakuwa na maana sana?

Ili upendo uwe na maana sio mpaka upokewe!Wenyewe umejitosha!
 

Dearest Kaunga naona wewe na baadhi ya wachangiaji hamjaelewa eiyer anaongelea upendo gani.
Haongelei mapenzi ya mwanamke na mwanaume.
Mi nimeelewa kuwa anaongelea upendo wa binadamu kwa binadamu wenzake kama jirani,rafiki,ndugu.
Kwamba kuna watu wanajiona wanadamu ya kunguni kutopendwa na hata mtu mmoja lakini wao wenyewe hawatimizi wajibu wao wa kuwapenda wengine wao wanataka wao wapendwe tu.
Cheki alivyosema hapa chini namquote

"(hapa nazungumzia kupenda kuliko zaidi ya ule wa ngono)"
 

Nimekuelewa queenkami na nilimuelewa Eiyer pia, just wanted to be specific kwa aina hiyo ya upendo (mapenzi ya wapenzi aka mume na mke) coz huko ndiko ninapopata tatizo mimi.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…