Hivi ndivyo itakavyokuwa pale unapoanza kufa

Hivi ndivyo itakavyokuwa pale unapoanza kufa

The dumb Professor

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2023
Posts
852
Reaction score
1,978
  • Nguvu za mwili zitaanza kukuishia,
  • Utasikia kama usingizi mzito unakuja,
  • Mapigo ya moyo yatapungua kasi,
  • Hali ya kukata tamaa kupigania uhai itakujia.
  • Utawaza maisha Yako tangu kumbukumbu za utoto wako mpaka hapo ulipo.
  • Utawaza mambo mabaya na mema uliyoyafanya/yaliyokutokea.
  • Utawaza vitu ambavyo ulipaswa/hukupaswa kufanya (mf. kama kutohudhuria mazishi ya mama ako, au kutomhudumia mzazi ipasavyo)
  • Utawaza mipango Yako yote uliyokuwa nayo ya future
  • Utawaza ukiondoka utaacha kumbukumbu gani? Na je ni % ngapi ya potential/uwezo wako umeitumia duniani?
  • Utawaza je vile vitu ulivyoviona vya thamani duniani (mf. pombe, wanawake, Simba na yanga)vina thamani kama ulivyovipa?
  • Utawaza na vile vitu ulivyovidharau na kuona havina thamani kama ulivyodhania (mf. mahusiano na ndugu/jamaa, dini, kufurahia maisha nk.)
  • Utawaza sana yote haya na utakosa jibu, kisha utaona kuwa vyote vizuri na vibaya ni ubatili mtupu na havina maana yeyote.

- Utapata hisia ya kukata tamaa ya kupata majibu kuhusu haya kipindi mwili wako unazidi kuishiwa nguvu,Mapigo ya moyo yanazidi kupunguza,pumzi inakuwa ya tabu na hali ya usingizi inaongezeka.

Hapo ndipo utakata tamaa na kukubali matokeo, kisha utakubali kuachia pumzi Yako ya mwisho na ndipo utakufa.

(Hizi process zinaweza kuchukua anywhere from masaa machache hadi sekunde kadhaa kulingana na aina ya kifo utakachokufa)
 
Mkuu hongera kwa kufa maana umetoa ushuhuda wa moja kwa moja kwa kuwa umepitia hatua hyo muhimu.ngoja sisi marehemu watarajiwa mda wetu ukifika tutakuja kutoa ushuhuda hapa kama wewe ulivo fanya .barikiwa sana [emoji1488][emoji1488][emoji1488]
 
Back
Top Bottom