Hivi ndivyo nitakavyokuwa nabet, nahakikisha napata faida kila siku, nidhamu muhimu, tamaa inaua

Tamati

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2017
Posts
1,085
Reaction score
1,960
Habari ya Mwaka Mpya wa JF.

Kama kichwa cha uzi kinavyojieleza, baada ya wezi kuniibia vitendea kazi vyangu mnamo usiku wa 26/12/2019 kwenye mgahawa nilikuwa nimeuanzisha, kuanzia hiyo siku hadi leo bado sijaweza kurejea tena kwenye shughuli hiyo baada ya kukosa mtaji wa kuinuka tena hadi sasa maana nilikuwa bado sijaanza kupata faida. Mwanzo mgumu

Sikuwahi kubet kabisa, ila kuanzia katikati ya December mwaka jana nikiwa naendelea na shughuli ya mgahawa nilianza kubet kidogo kidogo kwa option ya WIN au DRAW pekee. Nikawa nabet kwa kuweka hela kidogo(nilianza na elfu 1 nikaweka kwenye akaunti ya beting) na kuitumia kidogo kidogo kwenye mikeka. nikawa nalose na kuwin ila lose ndio zilikuwa nyingi.

Kwa sasa nikiwa nyumbani na mwaka mpya ushaanza kuchanja mbuga bado ramani ya kurudi kwenye shughuli yangu haisomeki, nimeamua nibet ambapo nahakikisha kila siku napata faida japo kidogo kutokana na majibu yangu ya utafiti mdogo nilioufanya na ukatoa mbinu kama ifuatavyo.

1. Nitaendelea kubet kwa option ya WIN na DRAW pekee.

2. Nitakuwa nachagua timu 4 za uhakika, ambapo kati ya hizo, timu 2 zitakuwa za uhakika wa kushinda kwa asilimia 90+

3. Nitasuka mikeka 8 kwa kutumia hizo timu 4 nilizochagua, nahakikisha kila mkeka unaleta faida ya jumla ya hela nitakayoitumia kusuka mikeka yote 8. Nikitumia jumla ya Elfu 4 ambapo kila mkeka nitausuka kwa mia 5, mkeka lazima uzalishe kuanzia elfu 4 na mia 5 na kuendelea. Hadi hapo nitakuwa na uhakika wa kupata faida japo kidogo

Kwenye picha ni mikeka niliyosuka jana nilitarajia kuvuna kwenye mkeka mmoja na nilifanikiwa kuvuna. Pembeni ni thamani ya kila mkeka na mkeka namba 6 ulitiki.
 
Wewe sio wa kwanza wala wa mwisho kufikiri hivyo.
Betting ni bahati huna bahati lose ziko palepale una bahati utafaidika na betting.
.
Na kwa kukukatisha tamaa tu wengi wa waliowahi kufikiri betting itawainua au kuwatoa kimaisha hawajawahi kufanikiwa ila wale wanaobet kwa kujifurahisha ndio huwa na hizo ngekewa.
Mfano nina 500 nahitaji kununua kifurushi cha shilingi 2500 nitaiweka kwenye kamari lengo ni kupata shilingi 2000 fasta cha ajabu nitaweka na kula 500 nyingine ndani ya dk 3-10 kisha nitaweka yote ili sasa izalishe 2000 kitakachotokea hapo nitapigiza hadi simu
.
Unajua kwanini?
Muulize Dr Ricky
 
Betting ni sawa na motivation speaker, kwenye makaratasi oa kwenye field ni vitu viwili tofauti. Hizi ni timu zilizowahi kunichania mkeka zikiwa na odds chini ya 1.17 tena zikiwa home.
Copenhagen
Malmo
Maccabi tel aviv
Bado msiba wa man city kufungwa na norwich city, kufungwa nje ndani na wolves, kufungwa na man u nk.
Yote hiyo nakutahadharisha kutokana na option zako za direct win zilivyo na matokeo ya kikatili.
 
huko tushapita mkuu karibu kwa ushauri zaidi ila hyo mbinu ni risk mno in case mechi moja ikichana utakuwa umeloose mikeka si chini ya miwili pia mechi ya pili ikicha unakuwa umeloose mikeka mingine si chini ya miwili,hvyo hyo so solution mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…