Nasri A Kulemba
Member
- Oct 16, 2015
- 20
- 56
HIVI NDIVYO PAUL WA MATUMAIN ALIVYOONDOKA OLD TRAFORD .
kalamu ya Nasri Kulemba
“NImerudi nyumbani “ni maneno aliyoyazungumza kwenye kipande kidogo cha video ,huku akiwa amevalia jezi zake nyekundu tofauti na zile alizokua amezoeleka kuzivaa ndani ya misimu mitano nyuma .
Hii ilikua ni maudhui ya kuutambulisha ulimwengu sasa Paul Pogba ni mchezaji halali wa Man united,baada ya kudumu takribani miaka 5 akiwa na klabu yake ya Juventuns .
Kwa mara nyingine tena kijana aliyependwa Old trafford anareje akiwa timamu na mkomavu ,akiwa na mataji manne ya Serie A, pamoja na Coppa Italia mbili na mataji mawili ya Supercoppa Italiano.
Bila shaka Manchester United walikua wamemsajili kiungo bora na kijana barani ulaya kwa nyakati hizo ,furaha kwa mashabiki ilkua kubwa sana,kwanza walikua hawajapata kiungo mahili kwa muda mrefu toka Paul Scholes atundike daluga … pili ni furaha kumuona kijana wao waliomlea anakuja kuitumikia klabu yao kwa mara nyingine baada ya kuondoka Old trafford kwa sinto fahamu .
Paul anashuka United anaikuta ipo katika nyakati ngumu za kiushindani ,licha ya hisia za upendo washabilki waliomunesha lakini bado walikua na matumaini nae makubwa;kupitia yeye United itarudi katika zama za ushindani kama awali .
Hisia hizi kutoka kwa mashabiki dhidi ya pogba ndizo zimefanya mwisho wa safari ya Paul Pogba pale United uwe ni wa kufikirisha .
Achana na kiasi cha pesa ya usajili iliyoweza kuvunja record ya dunia,Paul ni mtoto pendwa pale United,aliimbwa na hata pale mtu alipokuja na kumkosoa bado mashabiki walifumbia macho na kundelea kumkumbatia .
Nakumbuka mara kadhaa Jose Mourinho aliwahi kumshutumu Pogba ,lakini bado washabiki walimuona Josse ndiye tatizo zaidi,walimuhukumu Josse kwasababu hulka yake ni muongeaji !!!! sijui…lakini hawakutaka kumsikiliza na wakaendelea kumuamini pogba .
Walikua sahihi kuamini mbinu za Mourinho zilikua ni hafifu kuweza kumfanya pogba awe mahili uwanjani ,waliamini katika kipaji cha Pogba kutokana na kile alichokifamya akiwa Juventus .
Imani ya mashabiki wa united ilikua ni kubwa na waliamini Paul anavitu zaidi tofauti na hicho wanachokiona uwanjani chini ya Mourinho,kisha Mourinho dhidi ya Pogba akawa kafara na kuweza kutimuliwa,ungeewambia nini mashabiki wa Man united kuhusu Pogba !!walimpenda haswa .
Imepita takribani miaka 3 toka Jose Mourinho aondoke na imepita takribani miaka 5 toka Paul ajiunge na man united ,hakuna mabadiliko yeyote kupitia kwa klabu mpaka kwake Paul mwenyewe,alikuja akiiukuta Manchester united kwenye mashindano ya Europe league na anaiacha ikiwa europa league .
Leo Man United wametangaza kuachana na Pual Pogba ,hakuna shabiki yeyote wa man united aliyeshtuka,wala hakuna anayejali ..kila kitu kwa Pogba kimekua ni kawaida,matumaini yamekatika kwasababu chini yake hajawaonyesha kile ambacho walichokitarajia na wala timu hajafika lengo zaidi ya kuendelea kushuka.
Pogba anaondoka zake Man united na sijui kama atarudi tena ,Kila upande umemaliza hamu na kubaki na majuto… Pogba anaamini alifanya kosa kubwa sana kujiunga na Man United ,na United wanaamini hakuna faida yeyote walioipata kupitia Pual zaidi ya hasara na mabishano dhidi ya wakala wake Pogba marehemu Mino .
Hivi ndivyo United na Paul walivyomalizana, kutoka kusajiliwa £ 89.5 million mpaka kumuachia kuondoka akiwa mchezaji huru ,kutoka kuwa tumaini la mbadala wa Pul scholes na sasa wanamuacha ili waende kutafuta kiungo mwingine . Kuna sehemu apakuwa sawa kwa upande wa Pogba mwenyewe.
Kwa heri ya kuonana Paul Pogba ,kutoka kuwa tumaini jipya mpaka kuwa makaa ya mawe old tarafford.. Nadhai hata yeye haamini ;mambo yamebadilika ghafla.
Asante sana ,hivi ndivyo ndoa yako na Man United ilivyohitimishwa.
Instagram Nasri kulemba .
0753219535