SoC02 Hivi ndivyo unavyoweza kujiongezea thamani

SoC02 Hivi ndivyo unavyoweza kujiongezea thamani

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Jun 27, 2020
Posts
6
Reaction score
4
Na; Mashaka Siwingwa

Hata siku moja isitokee mtu yeyote akuambie kwamba mafanikio katika maisha ni rahisi. Majaribio ya kutimiza ndoto za mtu ni vita kubwa sana.

Ni vita ambayo kila mtu anatakiwa kupambana bila mipaka. Hii inatokana na ukweli kwamba vipo vitu na wapo watu mbalimbali ambao wanakuwa wanapambana kuhakikisha kwamba hufiki popote. Bahati mbaya zaidi ni kwamba hata rafiki, ndugu na jamaa zako wa karibu wanaweza kuwa chachu ya kuhakikisha kwamba wewe hufiki popote.

Njia mojawapo unayoweza kuitumia kufanikisha ndoto zako ni kwa kujiongezea thamani dhidi ya washindani au adui zako. Unaweza kujiongezea thamani wewe binafsi au kampuni au taasisi au biashara yako. Hii ni njia nzuri sana ya kuhakikisha unabaki kwenye mstari na ndoto zako zinatimia.

Hakikisha unatengeneza mazingira ambayo yatawafanya washindani wako katika biashara au shughuli yako ili kuwafadhaisha washindani au adui zako ambapo itawafanya wao wakuone wewe ni wa thamani zaidi yao.

Kujiongezea thamani na kuonekana bora kila kuitwapo leo hakuhusiani kabisa na madhaifu uliyonayo. Ni sahihi kwamba kila mtu ana udhaifu katika jambo fulani lakini haimaanishi sisi sote tunajua madhaifu ya kila mmoja wetu.

Ukweli ni kwamba mshindani wako anapata zaidi nguvu mara baada ya kujua kwamba wewe una udhaifu gani. Sasa hutakiwi kufanya makosa ya washindani wako kujua udhaifu wako kama unataka kuonekana bora kuwazidi wao.

Hali hii itawafanya wakuone wa thamani na kamwe hakuna anayeweza kukudharau au kukufananisha na vitu ambavyo siyo hadhi yako.

Fanya hivyo pia kwa kujifunza ustaarabu au ujuzi mpya kila siku ili kuwafanya washindani wako waendelee kubaki nyuma kila iitwapo leo. Ukitengeneza thamani yako kila siku unatengeneza mazingira ya wewe kuonekana bora na wa maana zaidi kuliko washindani wako.

Kumbuka; usishindane nao bali jiongezee thamani dhidi yao.

Ahsante sana!

Mashaka Siwingwa
Morogoro - Tanzania.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom