Hivi ndivyo wafugaji wengi wa kuku wanavyotapeliwa kwa kuuziwa vifaranga vya uzao wa pili au tatu

Umesema ukweli na asante sana kwa somo zuri.
Jambo la muhimu sana si kuweka ukomo wa mawazo kwamba lazima mfugaji anunue Kuroiler kutoka kwa AKM Glitters.

Msisitizo unatakiwa uwe kama unataka kufuga kuku wa Kuroiler unatakiwa ujiridhishe kama msambazaji/mfugaji anayekuuzia vifaranga wa Kuroiler ana cheti cha ithibati kutoka Kegg Farm India ambao ndio wazalishaji na wasambazaji wa Kuroiler wazazi duniani.

Pia wafugaji wanaotaka kuuza vifaranga wa Kuroiler inatakiwa wapate mafunzo kutoka Kegg Farm, wafanyiwe majaribio ya ubora kisha wapate cheti cha ithibati ya kusambaza vifaranga ambao ni F1.

Tuache kuibia watu na kiwadhulumu kwa kuwauzia vifaranga ambao sio uzao wa kwanza.

Ukihitaji kujua zaidi nicheki 0768678122.
 
Hayo makampuni makubwa yanayosupply hivyo vifaranga ni yaoi hayo ? Mtu ayataje please
 
Halafu guys Hivi TANBRO na KUROILER wakikuwa wakubwa wanafanana uzito au Kuna ambaye Huwa anakuawaida ya kuwa na uzitio mkubwa kuliko mwengine ? (Assuming wote wamelishwa vizuri)
 
Ukiongelea silverland unaongelea ipi? Waliopo mikoa yote? Au wa dar pekeake?

Kimfano wapo silverland pale nzuguni dodoma nao wanazalisha vifaranga ila unakuta kuku wengine ni wazuri wazito na wanapendeza, wengine kama wakienyeji wepessii na wengine vishingo na wengine ni vifupi vinene, kwa ufupi ktk kuku 100 unakuta ndani yake kuna makundi 3-4 tofauti.

Au ndo kawaida tu kupata mchanganyiko?
 
OS Cordis
silverland wanauza broiler?na kama sio silverland naweza nunua wapi ili kupata matokeo bora zaidi?
kati ya broiler na kuloirer(kwa mayai) kama mtaalam unamshauri mtu afanye option ipi?

unawaongeleaje sasso?mkuu pm....[emoji120]
Nasikia sasso wanakula sanackwa kuku 1000 wanaweza kula kg 130 kwa mwez kuroiler anakula kg 75 kwa mwez na mayai kuroiler wanataga vizur kuliko sasso ila sasso wako vizur kweny nyama sasso anaweza kufikia kg 1.5 ndan ya miez 3

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe umetumwa kwa niaba ya makampuni makubwa ili kuwahujumu wazalishaji wadogo. Mfugaji usiyumbishwe.
 
aksante kwa kutusambazia maarifa-tronics
 
 
kuna Kuku wapo Tunduma sogea karbu na shule ni wakienjeji pure kbs wanafika had 5Kg ila bei yake ni 35000+
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…