Uchaguzi 2020 Hivi NEC walimuita Magufuli na Kumhoji juu ya kauli ya "Mkurugenzi nakulipa mshahara, nakupa gari halafu umtangaze mpinzani!!"

Nkobe

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2013
Posts
2,204
Reaction score
3,277
NEC imemuita mmoja wa wagombea Urais kutoka chama fulani cha upinzani kumhoji juu ya kauli zake kwenye kampeni za uchaguzi, hivi kwanini hatujasikia NEC ikimuita na kumuhoji Rais Magufuli pale alipowataka wakurugenzi wasitangaze wapinzani hata kama wameshinda?
 
Kuna miiko na maadili ya uchaguzi!
 
Tatizo ni kutokuwa na katiba mpya na tume huru ya Taifa ya uchaguzi.

IRP. Benjamin Mkapa.
 
Hivi hii aliisema wapi?, kuna mtu anataka ushahidi hapa
 
Utaanzaje kumhoji mtu wakati nawe unamsaidia kufanya vitendo hivyo.
 
mkuu nec ni taasisi ya rais/ccm. Hawawezi kumuhoji mtu aliyewaajiri wakati bado wanaupenda mshahara. Tanzania haya ya sijui nec ni kiini macho hakuna tume pale ni janja janja hata raia wasipo mchagua mwajiri wao lazima watamtangaza kashinda!
 
Hii kauli aliitoa kabla ya kusign kitabu cha maadili !! kauli hii tunaiweka pending ingawa bado imo kichwani mwa watanzania wengi sana.
 
Tunaomba ushahidi na wengne tujue jamani hii kauli, mwenye nayo aiweke wengne hatujui alisema lini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…