Hivi NECTA examination ni kipimo sahihi kwa mwanafunzi?

Hivi NECTA examination ni kipimo sahihi kwa mwanafunzi?

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Wadau hivi ni sahihi kumpima mwanafunzi aliesoma miaka 4 kwa mtihani mmoja tu wa NECTA?Kama ni kigezo sahihi inakuwaje kwa mfano mtu anapata division 1 kidato cha 4 alafu mtu huyo huyo anakuja kupata division 4 katika mtihani wake wa kidato cha sita na sio kama mwanafunzi huyo alizembea kidato cha sita.Mfano mwingine ni pale mwanafunzi anapofaulu vizuri kidato cha sita ila akifika chuo kikuu anaishia kupata discontinuation.Na wote hawa wanakuwa na juhudi kama awali ika wanafeli tu ingawa kuna wengine hufeli kwa kutokusoma au kubweteka Hapa tuangalie wale ambao wanaendelea na juhudi ila bado wanafeli.

Kwa hali hii haiwezekani kuna kufaulu kwa bahati tu kutegemea na mtihani ulivyotungwa?Na je haiwezekani kuwa kuna kufeli kwasababu vitu vichache ambavyo mtu hakuvisoma ndio vimetoka kwenye mtihani na hivyo kuishia kufeli?Je kwa mazingira kama haya ni sahihi mtihani mmoja kuwa kipimo kwa mtu aliesoma kwa miaka yote 4.Swali lingin hivi nchi zote duniani zinatumia utaratibu huu?

Utaratibu wa vyuoni wa kusoma kwa semester na kuhusisha course work haufai kwa elimu ya sekondari?
 
Kuna kitu kinaitwa cumulative results zinazopelekwa NECTA kutoka mashuleni. Sasa kama huwa zinatumika kutoa judgement au la ni jambo jingine.
 
Back
Top Bottom