Hoteli kubwa yoyote wanachoangalia zaidi ya lolote ni guarantee ya wewe kuweza ku-deliver., jambo ambalo linawashinda wengi, sababu wakikwambia tunataka mayai kadhaa kwa siku hawategemei kesho yaje uwapigie simu sijui kuku wamekufa au leo nimepata nusu...
Ndio maana watanzania wengi wanashindwa hata kupata tender sehemu kama migodini, na wenzetu wakenya ni wajanja wana-form Ushirika na wanaomba na kuuza mayai yao kwa pamoja.., sababu hapo wanakuwa na guarantee wa kuweza kupata idadi yoyote ya mayai siku yoyote. Kwahio kama kwenye hoteli kubwa ukiweka contract ya kuwapelekea mayai 500 kila wiki lazima upeleke hayo 500..., ndio maana nikasema huenda kwenye hoteli ndogo, ndogo au migahawa ila kama unao uwezo wa kukidhi deliver ya mayai kiasi fulani bila kukosa nenda to kwenye mahoteli ongea na watu wa manunuzi kama bei yako ni product yako ni safi sioni kwanini wasikupe tender..
Kama huwezi ku-guarantee kiasi fulani cha mayai basi ungana na wafugaji wenzako huko Morogoro tengenezeni ushirika na muuze kwa pamoja.., yaani kila mfugaji chochote anachokipata anapeleka kwenye ushirika alafu huo ushirika ndio unatafuta tender. Na hii itasaidia hata kununua vyakula mkinunua kwa pamoja mnaweza mka-bargain bei..
Sio kwamba mimi ni mfugaji.., bali am Jack of All Trades and Master of Non..... "kwahio ninapenda kufuatilia how things works"