Hivi ni kwa nini mganga hajigangi?

Top Gun

Member
Joined
Dec 11, 2024
Posts
49
Reaction score
171
1: Kwa maana hana uganga wowote ni utapeli tu.

2: Kwa maana maagano yake hayamruhusu kujiganga

3: Anaogopa matokeo ya uganga huo kama akijisaidia binafsi
 
Huo msemo wa mganga hajigangi unahitajika kufafanuliwa ili ileweka vizuri tafsiri yake hajigangi kvp? Kwa sababu nijuavyo mganga kuna baadhi ya mambo humtokea hivyo anatakiwa kujitibia mfano unakuta mganga wakati mwengine hupoteza baadhi ya nguvu zake za kiganga au mambo ambayo huathiri kazi zake za kiganga hivyo hujiganga.

Kuna wakati mganga hujifanyia dawa ili kuvuta wateja na kuboost mambo yake ya riziki kwa ujumla.
 
Sawa mkuu
 
Atajichanjaje chale Kati Kati ya UTI wa mgongo,au kama anaumwa hawezi kusimama atachinjaje kuku,Kisha hata daktari wa koti jeupe ni mganga pia anaweza kujifanyia operesheni?neno Hilo ni Pana.
Sawa sawa
 
1: Kwa maana hana uganga wowote ni utapeli tu.

2: Kwa maana maagano yake hayamruhusu kujiganga

3: Anaogopa matokeo ya uganga huo kama akijisaidia binafsi
Masharti ni magumu hata Mwanaye wa kumzaa asingependa ayapitie.

Ndip maana anakutengenezea wewe wakati Mwenyewe ni Choka mbaya na watoto wake wamepauka balaa hadi kukonda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…