Hivi ni kwa nini ngono zembe ndiyo iko kwenye chati?

Hivi ni kwa nini ngono zembe ndiyo iko kwenye chati?

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
219,468
Reaction score
911,184
Pamoja na wadau wa kupambana na vvu kuibidiisha jamii iepuke ngono zembe yaelekea kizazi hiki kina laana fulani mbona hakisikii la mkuu?


Tena hakiogopi kuvunjika guu? Kuna nini?


Kasi ya uambukizaji wa vvu inapanda kila kukichapo na tafiti nyingi zinabainisha ni ngono zembe hivi kulikoni?
 
Katika mada zote nilizozipitia leo hapa JF ni hii tuu ndiyo yenye upevu na ambayo inatakiwa watu kuichangia kwa kila hali na si yale mambo ya ujinga ujinga wa watu kutaka kushika madaraka ili wao na familia zao wafaidike na mapochopocho huko ikulu.Ongera mkuu kwa kuleta mada iliyokwenda shule na wengine wajifunze toka kwako.
 
Tatizo hili linatokana na mambo mengi hasa Umasikini ambapo hali ngumu ya uchumi inafanya watu watumbukie kwenye ngono kwa ajili ya kujikimu. Ulevi wa pombe na madawa ya kulevya ni mojawapo ya matatizo yanayomfanya mtu aingie kwenye ngono zembe bila kujizuia. Swala jingine ni kutokana na kuporomoka kwa maadili ambapo watu hawana aibu na maswala ya ngono wadogo hawawaoogopi wakubwa na wakubwa MAFATAKI hawana haya kutembea na watoto wadogo ambao ni sawa na watoto wao.
 
Kuna mambo mengi yanayosababisha hali hii kutegemea na hali ya tendo lenyewe na mahali linapotendeka.Ila kwa mtazamo wangu kubwa zaidi ni kukata tamaa kwa watu na mwamko mdogo.Niliwahi kutembelea maeneo fulani ya mikoa ya kanda ya ziwa na kila patner niliyekutana naye alikuwa ananiuliza unavaa ya nini sasa unaniona mimi mgonjwa?Hapo ni mwamko mdogo na la kukata tamaa ni pale mtu anapoamua kutotumia kinga ilhali akijua kila kitu kuhusu maambukizi ya HIV .Kuna watu wanasema ni heri kufa kwa HIV kuliko kufa kwa njaa.Kwa maana hiyo mtu huyo anakuwa amekata tamaa na hajali chochote kuhusu maisha yake.Wengine wanakwenda mbali zaidi na kusema condom inapunguza utamu,sasa huwa najiuliza ni kipi bora utamu wa dakika moja au maisha yako ambayo huwezi kuyalinganisha na chochote hapa ulimwenguni kwa thamani?
 
sina hakika na takwimu zako. yaani ongezeko unalosema ni la kitaifa, kikanda,
kimkoa n.k? labda ungefafanua zaidi basi huenda majibu makini zaidi yangepatikana.

hata hivyo binafsi naamini mkakati unaotumika wa kukabiliana na tatizo hili
unawalakini. naamini mkakati wa kumtishia mtu katika haya masuala
hautafanyakazi. hebu fikiria kuna maumivu zaidi ya yanayosemekana yatapatikana
jehanamu? je tishio hili la jehanamu na moto wa milele limefanikiwa vipi
kuwafanya watu waache "dhambi" hususan ngono aka uzinzi na uasherati? lakini hii
ni mada nyingine ndefu zaidi.
 
sijui ndo global warming manye!! maana hata ukisema kondom je modomoni? mtu bila kula mate na kuzama uvinza na wengine kusema na mike bado hakieleweki, tutapona kweli hapo!!??
 
Katika mada zote nilizozipitia leo hapa JF ni hii tuu ndiyo yenye upevu na ambayo inatakiwa watu kuichangia kwa kila hali na si yale mambo ya ujinga ujinga wa watu kutaka kushika madaraka ili wao na familia zao wafaidike na mapochopocho huko ikulu.Ongera mkuu kwa kuleta mada iliyokwenda shule na wengine wajifunze toka kwako.
Futa kauli yako we kijana mdogo, siasa si mambo ya kijinga hata kidogo..anyway, tarehe ulizojiunga hapa zinakulinda uongee kauli kama hiyo!

Back to the thread, hali ya ngono zembe inazidi kuongezeka mitaani...na matendo mapya ya kifirauni yanazaliwa kila siku!
Halafu naona kama vile sasa hivi kampeni za kuhamasisha matumizi ya zana zimeenda likizo, au media zimejikita kwenye siasa nini?
Ni jukumu la kila mtu kupima hali hii, na kukemea pale anapoweza!
 
na sie binadamu kwa kutaka kujaribu kila kitu, tukiona tu kwenye movies za xxxxx na siye tunataka tufanye hivyo hivyo
 
Unajua mila na desturi zetu ni tofauti sana kuna jamii nyingine hazijui hata condom ni nini,, mf wamasai sasa hawa walinzi wanakuja town wanapata kazi then wewe unategemea wakipata mademu nini kitaendelea?????

hili somo linatolewa mijini tu japo napo huku mijini bado watu hawajabadilika kabisa....
 
Tatizo kubwa la vijana wetu au jamii kwa ujumla kuendeleza maadili machafu wala si kwa sababu ya umasikini, mimi ninachoona hapa ni elimu ya ukimwi ndio bado wengi hawana. Na lingine viongozi wetu wa dini ambao ndio kioo cha jamii wengi wao ndio wana maadili mapotofu hivyo hakuna tena kumhofu Mungu. Wengi wa vijana wetu wanaogopa wazazi once wanapokuwa mbali nao hufanya watakavyo na wanaona maisha ndiyo hayo, kwani elimu ya ukimwi katika ngazi ya familia ni ZERO.

Ushauri wangu ni taifa lijikite zaidi kuendeleza elimu hii ya gonjwa hili na pia watu wamrudie Mungu ili kale kahofu ka hukumu ijayo ya Mungu kawe ulinzi wetu.
 
Back
Top Bottom