sina hakika na takwimu zako. yaani ongezeko unalosema ni la kitaifa, kikanda,
kimkoa n.k? labda ungefafanua zaidi basi huenda majibu makini zaidi yangepatikana.
hata hivyo binafsi naamini mkakati unaotumika wa kukabiliana na tatizo hili
unawalakini. naamini mkakati wa kumtishia mtu katika haya masuala
hautafanyakazi. hebu fikiria kuna maumivu zaidi ya yanayosemekana yatapatikana
jehanamu? je tishio hili la jehanamu na moto wa milele limefanikiwa vipi
kuwafanya watu waache "dhambi" hususan ngono aka uzinzi na uasherati? lakini hii
ni mada nyingine ndefu zaidi.