Hivi ni kwamba bidhaa za mbao hazina thamani tena siku hizi?

Hivi ni kwamba bidhaa za mbao hazina thamani tena siku hizi?

Pendaelli

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2014
Posts
11,050
Reaction score
31,412
Wakuu heshima kwenu.
Nakumbuka 2005 kurudi nyuma feniture itokanayo na mbao ilikua ikihitajika kwa wingi na jamii.
Tofauti na siku hizi seramala amekua na thamani ndogo sana.
Hata vyuo vya ufundi fani ya seremala haina vijana kabisa.
Nini kimeikumba sekta hii ya mbao?
Wako wapi wateja wa makochi, vitanda, meza, milango, fremu, shata, meza za ofisi na viti vyake, na za chakula, kabati za nguo na za vyombo, shelvu nk?
 
Kwanza kabisa na la muhimu ni Uhifadhi wa Mazingira.
Pili ni bei zisizo na uhalisia na tamaa za mafundi ndio zimepelekea watu kuhamia kwenye samani mbadala wa mbao.
Kama wasingekua wanapeleka magogo nje miti ya mbao haiwezi kuisha kwa wepesi hivyo
 
Kama wasingekua wanapeleka magogo nje miti ya mbao haiwezi kuisha kwa wepesi hivyo
"Wasingekuwa" kina nani hao!?
Ukileta Siasa katika mambo ya msingi kama haya ambayo yanapaswa kujadiliwa kwa hoja nitakuona mngese wa kiwango cha SGR. Otherwise ungeweka hili bandiko lako katika jukwaa la Siasa kuna baadhi ya watu tungepita kimya.
 
Wakuu heshima kwenu.
Nakumbuka 2005 kurudi nyuma feniture itokanayo na mbao ilikua ikihitajika kwa wingi na jamii.
Tofauti na siku hizi seramala amekua na thamani ndogo sana.
Hata vyuo vya ufundi fani ya seremala haina vijana kabisa.
Nini kimeikumba sekta hii ya mbao?
Wako wapi wateja wa makochi, vitanda, meza, milango, fremu, shata, meza za ofisi na viti vyake, na za chakula, kabati za nguo na za vyombo, shelvu nk?

Nakumbuka nilikuwa nakitanda changu cha mbao,nikapata safari ikanibidi nirudishe vyombo nyumbani na kutudisha chumba nilichopanga,vyombo vyangu vikawekwa stoo.

Sasa baada ya kurudi safari nitakatafuta room nikapata sasa kimbembe kikawa kufungua stoo nakuta kitanda kimegeuka makazi ya mchwa,nikakichukuwa kibishi bishi.

Ebwana usiambiwe sikia tu kwa watu mchwa ni kama panya wakisikia wageni ndiyo wanaanza kula mbao sauti Yao inakera mbaya

Usipate demu mpya geto kosa wanaanza kusumbua ili mradi tu kero
 
Kungekuwa na utunzaji wa mazingira wachina wasingesafirisha magogo yetu na kuyapeleka kwao. Wanachonga samani na kuuzia nchi za magharibi.

Wafungwa wa Keko wangepelekewa mninga wangechonga meza na viti vya walimu pia madawati yawatoto wetu.
 
Old school kwa sababu hauafford au?
Ishu si ku afford tu, hivi kuna mtu anaweka TNG badala ya Gypsum kama cieling kwa sasa?

Ni wangapi leo hii wanaweka madirisha ya mbao nondo na wavu wakaacha kuweka grills za chuma na alluminium & glass ama PVC windows!

Na saingine gharama huwa juu kuliko hata mbao ambayo ni style ya kizamani.
 
Vyote ni bei chini hivyo
 
Usiseme mbao hazitumiki sema watu hawana pesa ya kumudu thamani za mbao.
Mimi ni mjenzi kila iitwayo leo natumia mbao kama kawaida, tatizo bei sio rafiki kabisa wakati wa kumwambia mtu bei unashikwa na kigugumizi ila ndio ukweli.
Bizaa zitokanazo na mbao ni bei mbaya mno ila zinavutia hakika ukikutana na watu makini wanaojua nini unahitaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom