Hivi ni kwanini benki za Tanzania hazimlei na kumuelimisha mteja?

African Believer

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2015
Posts
436
Reaction score
426
Natumai wana Jamvi wenzangu mu wazima wa afya tele. Kama ni wazima karibuni kwenye uzi wa malalamiko dhidi ya benki za Tanzania.

Kwa miaka mingi sasa nimekua mkopaji na mnufaika wa taasisi za kipesa hapa Tanzania hasa mabenki. Lakini cha kushangaza sijawahi patiwa elimu yoyote yenye manufaa kwa ajili ya mustakabali na ustawi wa biashara yangu.

Na badala yake mabenki niliyopitia yamekuwa yakiweka sheria zinazomkandamiza mteja, hasa pale biashara inapokua haiendi vizuri. Utawakuta wakilazimisha marejesho pasipo kutaka kumsikiliza mteja na kumpa ushauri ni nini cha kufanya ili aweze kuondokana na mkwamo unaomkabili.

Matokeo ya wakopaji kukosa malezi na elimu kutoka kwa mameneja pamoja na maafisa wengine wa benki wenye jukumu hilo, benki nyingi hapa nchini zimekosa ustawi kwani wateja wake wengi hujikuta wakishindwa kurejesha marejesho kulingana na muda uliowekwa hali inayopelekea kupoteza mali zao walizoweka kama (collaterals) dhamana.

Jambo hili limekua kikwazo cha muda mrefu na watu wanaogopa kukopa kutokana na kuona spidi ya watu kufilisiwa malizao na kupoteza makazi kwa kuuziwa nyumba zao walizoweka kama dhamana.

Najua kwenye jukwaa hili hawatakosa wawili watatu wakutueleza ni kwa nini hili limeendelea kuwa tabia ya mabenki yetu.

Karibuni wana Jamvi.
 
Nimeshakopa Bank na pia nimenufaika na mikopo kutoka na nidhamu ya pesa niliyokuwa nayo!na marejesho kwa wakati na Mara nyingine kabla ya wakati, mtoa mada usitegemee bank watakumbembeleza kwa namba moja ama nyingine, wapo ili wanafaike na mkopo waliokukopesha na wewe upo kwenye mkopo uliokopa ili unufaike!,sasa kumbembelezana kunatoka wapi!?
Pambana mtoto wa kiume usingoje huruma
 
Mkuu,kukopa ukope wewe,halafu benki wakupe FREE BUSINESS CONSULTANCY SERVICES? hapana, nawatetea,,,ni wajibu wako kuitafuta hiyo elimu kwa business consultants ambao wako dedicated kabisa for that cause!...mimi pia nafanya biashara nikikwama nawatafuta wataalamu wa biashara au kodi wananiahauri naendelea mbele....mkopo ukikwama mara nyingi huwa naandika goodwill letter to my banker na huwa wananielewa......benki huwa wakali kwa defaulters
 
Nakubaliana na mawazo yako, ila ni lazima utambue kwa sasa kuna wananchi wengi wakawaida (wa vipato vya chini) wanakopa. Benki zinawapa mikopo kidogo ambayo haiwawezeshi kwenda kwa hao business consultants.

Hivyo basi ili wakopaji wanufaike na benki ziendelee kupata faida ni lazima zikubali kuingia gharama ya kutoa elimu na ushauri kwa wakopaji/wateja wake.

Kumbuka pindi mkopaji anaposhidwa kunawiri ni changamoto kwa uchumi wa nchi ambapo mteja na benki vinakabilia na mkwamo ambao ungeweza kuepukika, kama elimu na ushauri vingetolewa.
 
Swala la kukopa na kunufaika ni swala mtambuka sana, pia benki hazifurahii pale mteja wao anaposhindwa kulipa.

Kumbuka hata ile collateral unayoweka ni kwa ajili ya security tu na benki haina nia ya kuichukua. Na pindi wakilazimika kupiga mnada kile kilichowekwa dhamana yaani inamaanisha hasara kwa pande zote mbili, yaani benki inakosa mteja na mkopaji anapoteza mali yake aliyoweka jama dhamana.

Mwisho utambue nimeanzisha uzi huu kwa sababu nimeshuhudia wakopaji wengi wakiteketea kwa kukosa nidhamu ya pesa ambayo wangeweza kuipata kutoka kwa walimu wao wa mikopo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…