Hivi ni kwanini 'CCM' hawataki Tume Huru ya Uchaguzi wakati wana wanachama milioni kumi na tatu?

NgerukeAbra

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2022
Posts
4,253
Reaction score
5,789
Wasalaam ndugu.

Sina kona kona nyingi cha msingi naomba kuelimishwa kwanini chama tawala na serikali yake hawataki tume huru ya uchaguzi?

Juzi kati chama hicho kilitoa taarifa kuwa kina jumla ya wanachama milioni kumi na tatu.

Pia kinajinasibu kuwa kimefanya mambo mengi ya maendeleo nchini.

Kwa vigezo hivyo viwili ni rahisi kwao kushinda uchaguzi hata tume ikiwa huru.
 
CCM Wana hela za wizi kuhonga wapiga kura na kuwasafirisha kwenye.malori usahwishi wa kushinda uchaguzi hawana
 
Wanajua wao ndio tume huru ya nchi, Wanahisi wananchi hawaitaji chochote zaidi ya CCM, kwa kipindi chote walichomiliki nchi wameongeza fursa za michezo ya kamari kuliko Fursa za Elimu Bora
 
Mimi mwenyewe ni mwanachama wao na Nina kadi ya kidigitali ila wakinitizama sana wanaona kabisa sifananii na wao..wanaingiza hofu😀😀. Wapo wengi ambao wapo ndani na hawapendi baba yao awanyanyase majirani, mara awapige majirani....watoto walioko ndani si wote wanaipenda uonevu..utawaona sura zao tu. Ccm hawawezi kujiamini kwa matendo wanayoyafanya wenyewe, shetani hawezi kuwa na nguvu kwa Mungu...hata Mungu asipotamka lolote akatizama tu...utaona mtu akichanganyikiwa....ndivyo chama chetu kilikofikia..hakuna ujasiri tena
 
Eti?
Bila kusau mama kafanya mengi
-Mama anatosha
-mama hana deni
-Mama anaweza
-mama kafungua nchi
-mama hana baya
-mama anamwaga mabilioni
-mama katoa ajira kwa kila muhitaji
-mama kafanya hospitali zikose wagonjwa
-mama.........
-mama.........
-mama.........
-mama.........
-mama.........
-mama.........
-mama.........
-mama.........
 

Matokeo ya uchaguzi huru, wa haki na wenye kuamininika wanajua hawawezi kutoboa.
 
Watashindwa Saa Nne Asubuhi Kuku Wanaona
 
Ndio kichinjio chao
 
Hiyo taarifa ya wanachama 13m ni kukuandaa kisaikolojia kukubali kuibiwa kura, kwa maana watasema sisi tuna wanachama 13m na wote wamepiga kura.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…