Hivi ni kwanini kila msanii anayefanya Collabo na Diamond hupotea kwenye game mazima?

AdvocateFi

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2012
Posts
11,492
Reaction score
5,047
Habari wakuu!
Leo nimeamua kuleta hoja hii mezani ili tujadili maana swali hili nimelifanyia utafiti kwa muda mrefu,

Je ni kwanini kila msanii anayethubutu tu kufanya collabo na Diamond AKA simba jini roho mbaya, huwa anapotea kimziki mazima, Je tatizo ni nini?
Inamana uwezo wa Diamond ni mkubwa kiasi kwamba kila anayefanya naye collabo baada ya hapo huonekana kufunikwa hadi kupoteza radha ya kimziki?
Au je ni ndumba kama ule uvumi wanaosema ukiimba na Chibu basi hapo hapo jamaa huiba nyota yako? Jibu mnalo wenyewe.
Lakini iufuatayo ni baadhi tu y mifano ya wasanii waliokumbwa na kadhia hii mbaya.

1. Hawa
Msanii huyu kuna kipindi miaka ya 2009- 11 alikuwa miongoni mwa wasanii wakali wa kike hapa nchini , Alifanya collabo zuri na Chibu [HASHTAG]#Nitarejea[/HASHTAG] ila baada ya hapo kapotea, sasa hivi anakula hadi unga, daily kulalamika kwenye media kuwa katengwa.

2. Chidi Benzi
Huyu alikuwa rapper the top hapa Tz na East Africa, Alishirikishwa na Mondy kwny wimbo [HASHTAG]#Nalia[/HASHTAG] mengi na wimbo ulikuwa mkubwa sana ila baada ya hapo kilomchotokea Chidi mpaka leo wote tunakijua.

3.Davido (Nigeria)
Huyu jamaa alikuwa hot cake kwa Africa hasa 2013-2015 ila baada ya kuimba [HASHTAG]#NumberOneRemix[/HASHTAG] na Diamond jamaa kapotea mazima hadi leo.

4. IYANYA ( Nigeria)
Naye huyu hatofauian sana na Davido, baada ya kuimba na Simba [HASHTAG]#Bumbum[/HASHTAG], huyu jamaa mpaka leo kabaki historia, naskia now ni fundi garage huko Nigeria

5.Bracket (Nigeria)
Aliimba na Mondy na wimbo wa [HASHTAG]#Alive[/HASHTAG] ila baada ya hapo hajulikani mziki kaacha au vipi
6.KCEE (Nigeria)
Huyu naye alivuma sana ila baada kutoa ngoma na Simba, [HASHTAG]#Loveboat[/HASHTAG] kapotea mazima

7.Mafikizolo
Hawa ndo kabisa hatujui sasa hivi kikundi chao kimekuwa sacoss au vipi, wamepotea mazima, sautsol wamechukua hadi nafasi yao.

8. Harmonize
Huyu dogo alikuja vizur na Aiyola, iila baada ya kuimba [HASHTAG]#Bado[/HASHTAG] na hili jini roho mbaya, dogo kapotea anabaki kuimba matatizo sjui ujinga gani sasa, na kusikika kwa kiki za mapenzi.

9.Linex
Huyu jamaa tangu kaimba Salma na Diamond, leo hii kabaki historia

10.Linah sanga
Mamawee hapa ndio nikae kimya, tangu ile kizaizai remix kapotea mbaya

11. Nay wa mitego
Namkubal sana huyu jamaa ila tangu aimbe mziki gani na chibu, simuelew kabsa ngoma zake siku hizi
12.Psquare
Tena hawa ndio wanatia huruma, wamebakia jina tu

13.Neyo (USA)
Huyu nyota ilianza kung'aa alipokuwa karibu na Kingkiba ila tangu apige collabo na Chibu bin awards, lol pole yake anatia huruma

14.Shetta
Mzee wa my New ride, pole baba, simba hapendagi ujinga ujinga.

15. Raymond
Mmh huyu ngoja tumpe muda, ila kuimba salome na Simba, nahisi ndiyo kachuma janga, let's watch out.

My Outlook: je tatzo nini, kweli kafara ya kubebeana nyota haihusiki hapa au nature ya game tu lenyewe halipendagi ujinga ujinga?

Bye.
 
Umesahau shetta,linex na yule muimba taarabu.....[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2] watu wapo kazin aseee
 
Dully Sykes Alisha imba na plutnumz je nae kapotea? Mr. Blue nae alikwisha imba na Diamond je nae kapotea? Ali Kiba Alisha imba na Mond (Lekaditugite) vipi na yeye kapotea? pia Prof Jay Alisha piga Collabo na Baba Tiffah nakuuliza naye kapotea? Usisahau A.Y amekwisha dondosha collabo na mtoto wa Tandale nae vipi nae kapotea? Ngoja nikukumbushe tena , je 'wacha waoane' unajua ni collabo ya ngapi ya Chege na Mondi, vipi mtoto wa mama Saidi kapotea? Vipi kuhusu wale mapacha P-square wamepotea nao baada ya collabo na Simba? Hahahahahahaha bila shaka ile 1 ya 4 itakuwa inafanya kazi maeneo ya huko uliko...
 
Una angaika sana

Kama n mjani unatumia basi mjani n compatible kabsa kwako ...
 
watu warambe miunga yao huko alafu useme kapotezwa, kama kuroga na wao si wakarogeee? au una uhakika gani kama wao hawarogi?
 

Mkuu anzisha thread mpya tutachangia, ila hapa naomba tujikite kwenye hoja hapo juu
 
watu warambe miunga yao huko alafu useme kapotezwa, kama kuroga na wao si wakarogeee? au una uhakika gani kama wao hawarogi?

Mkuu nineweka kama swali, sijasema direct kuwa fulan karoga au karogwa.
 
We jamaa unahangaikaga sana. Maana unaacha kumsupport msanii wako kutwa diamond mdomoni mwako. Wewe unaonekana unampenda sana mondi yan ukilala unamuota. Haiwezekan m2 huyo huyo daily unamuongelea.

Kwahyo diamond ndo aliwatuma chidi n hawa kutumia unga?

Diamond ndiye kiungo huko sony anayezuia nyimbo za davido?

Hlf bracket mbna hawa kumshirikisha diamond peke yake kuna Tiwa Savage pia.
Kwel ni 1/4
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…