wewe nini kimekufanya useme chanzo cha ugomvi ni mwanamke?
nakubaliana nawe kuwa wanaume wengi wakishaoa huwa maelewano mazuri na ndugu zao yanapungua, ila sidhani kama tatizo huwa ni mke.
nakumbuka kuna kaka yetu alikuwa bonge la mshikaji kwetu (kabla hajaoa), yaani akitokea tu kila mtu anatabasamu maana unajua shida zako zoootee zinakaribia kuisha. alipooa kuna vitu vikaanza kupungua, walipopata mtoto ndo kabisaaa, na kuna kipindi alikuwa mkali kweli ukitokea na shida yako. sasa karibu kila mtu akawa anamchukia wifi (siyo kaka), eti ndo anamfanya awe mkali wetu. ila mimi nilikuwa namwonea huruma sana wifi, siku nikamwambia kaka kuwa huku wenzako hawampendi mkeo, anakufundisha usitujali. kaka akatukalisha kikao, kuanzia mama mpaka wote, akatuambia kuwa kabla hajaoa hakuwa na majukumu ya kifamilia ndo maana aliweza kutufanyia kila tutakalo, ila sasa ana majukumu mengi; mke, mtoto, wakwe......... so tusimlaumu mkewe pale anaposhindwa kutufanyia baadhi ya vitu