AbuuMaryam
JF-Expert Member
- Dec 26, 2015
- 2,577
- 4,637
Feisal angekuwa sasa hivi ni lulu Africa, naamini miamba ya nchi za Kaskazini na zingine za Kiarabu au hata za Ulaya zingekuwa zinammulika kijana huyu akikiwasha ligi ya ndani na kimataifa.
Hivi alishindwa nini kusubiri huku akiwagomea Yanga kusaini mkataba mpya, naamini kuna timu za maana kama Al Ahly zingesema sina mhitaji, zisingeshindwa kulipa pesa yake anayotaka yoyote ile kuliko hiyo aliyodanganywa nayo iliyomfanya kuwa mtumwa, kiasi kwamba atabidi akae nje hachezi popote mpaka mkataba uishe.
Feisal ungeziba tu maskio ukawa Prof, ukaendelea kukipiga Yanga huku umewagomea Yanga kusaini mkataba mpya. Goma kabisa kata kata, either uuzwe au usubiri mkataba uishe. Naamini wangekuuza tu.
Sasa sijui unapata nini, zile hela ulizodanganywa nazo bado zipo? Huenda aliyekudanganya alitumia ile mbinu ya ukitaka kumdhoofisha adui yako iba katika silaha zake muhimu, hawakujali mustakabali wako wa kisoka.
Mama yako alilalamika kuwa mwanae ajira yake ni mpira, sasa hivi mwanao ni mpira gani mwanao anaoucheza?
Sawa bila shaka mama ulimtakia mwanao mema, ila sio kila jambo tunatumia hisia na mapenzi, muda mwingine tuwaache wenye maarifa watumie maarifa yao, na huko ndiko kumtakia mema.
Sawa, yanaweza mambo yake yakaisha kabisa akarudi kucheza soka kama kawaida, je, tuna uhakika kiasi gani Feitoto atarudi na kiwango kilekile alichomalizia Yanga? Atakuwa bora vile vile au ndio tutakuwa tumempoteza kama Ibrahim Ajibu, Ramadhani Singano Messi, Deo Kanda, Mrisho Ngasa, Gadiel Michael na wengineo waliojiharibia mustaqabali wao wa soka kama wewe Feisal?
Nakuonea huruma kweli, kama jambo hili limenikuta mie. Huenda sasa hivi tungekuwa kila sehemu Afrika inaimba jina lako Feitoto, huku mkataba na Yanga unaenda ukingoni na wakati huo unakiwasha, na umegoma kusaini mkataba mpya, wataka kwenda tu.