Sio kweli,nina mshikaji wangu anafanya hizo shuguli japo yeye bei zake kwangu tofauti na wengine.
Mfano wakati nataka kuweka milango 2 ya Aluminium ya futi 8/8 kwenye frem,mafundi niliowapeleka wa kwanza alitaka 700k kila mlango tukaongea mpaka bei ya mwisho 650k,wa pili 750 akaja mpaka 700k na watatu alisema 650k tukaja mpaka 600k...kipindi hiko jamaa alikua amesafiri na mimi nina haraka ila nilivyoona pesa inafika 1.2M ukiplus na mlango mdogo 300k ikabdi niwe mpole kumsubiri.
Aliporudi mlango mkubwa aliniwekea kwa 425k kila mmoja na mdogo 210k ,,hapo ndo akanambia amepata faida ila sio kubwa sema huwa wanaweka bei kubwa zaidi maana hizo kazi za msimu.