Habari za saa hizi, wadau. Nimepata tatizo, nikasema nililete hapa JF kwa wadau ili nipate suluhu. Maana JF ni uwanja mpana, na kwangu mimi imeshanitatulia mambo mengi sana ambayo hata sikuomba ushauri.
Mimi nilinunua kiwanja. Kiwanja hicho hakikuwa na hati, lakini tayari kishapimwa. Process zote za kutengeneza hati nimezimaliza ila jambo moja tu ndilo limebakia: swala la ramani ya mipango miji.
Niliwaambia mbona pameshapimwa na copy ya ramani nilileta. Wakaniambia bado ramani ya mipango miji. Kilichonishangaza ni gharama zake. Nimeambiwa ni milioni 3 kupimiwa ramani ya mipango miji. Mwenyekiti anadai pameshapimwa tayari, lakini nikiwaambia wanasema ramani hiyo siyo ya mipango miji. Sijui kisheria ramani zinatakiwa ziwe ngapi. Hawataki kuniambia katika hiyo milioni 3, ya serikali ni ngapi.
Nahitaji msaada wa kujua gharama halali ya kupimiwa ramani ya mipango miji kwa kiwanja ambacho urefu na upana wake ni 20/40. Halafu ni kiwanja cha kujenga nyumba moja tu na eneo dogo la uwani, lakini bei ya kupimwa utasema nimenunua shamba. Nataka nijue gharama ya ukweli; sina shida kuwapa posho yao, hata iwe laki tatu.
Wizara ya Ardhi